Post Details

UJENZI WA VITUO JUMUISHI VYA UTOAJI HAKI WASHIKA KASI

Published By:LYDIA CHURI

Na Lydia Churi-Mahakama

Ujenzi wa Vituo sita Jumuishi vya utoaji haki unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini ambapo majengo hayo yanatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi kumi.

Mahakama ya Tanzania inaendelea na ujenzi wa majengo sita ya vituo hivyo katika mikoa mitano nchini ikiwa ni hatua ya kutatua changamoto ya upungufu na uchakavu wa majengo ya Mahakama. Mikoa hiyo ni Arusha, Mwanza, Dodoma, Morogoro na Dar es Salaam katika wilaya za Kinondoni pamoja na Temeke.

Majengo hayo yenye sakafu nne yaani gorofa 3 yameanza kujengwa mwezi Januari mwaka huu na yanatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 10. Aidha yatajumuisha ngazi zote za Mahakama kuanzia Mahakama Kuu mpaka Mahakama ya Mwanzo pamoja na ofisi za baadhi ya wadau wa Mahakama wakiwemo Polisi, Ustawi wa Jamii, Mawakili na Waendesha Mashitaka.

Kusudi la kuweka ngazi zote za Mahakama ndani ya jengo moja pamoja na ofisi za wadau ni kurahisisha mchakato wa upatikanaji wa haki pamoja na kumpunguzia mwananchi gharama.

Majengo haya yanajengwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia. Lengo la Mahakama ni kuwa na huduma ya Mahakama Kuu katika kila mkoa, Mahakama za Hakimu Mkazi katika kila Mkoa, Mahakama za Wilaya kwenye kila Wilaya na Mahakama za Mwanzo kwenye kila Tarafa kulingana na upatikanaji wa rasilimali fedha.

 

 

Comments (0)

Leave a Comment