Post Details

JAJI KIONGOZI ATAKA KESI ZA JINAI KUSIKILIZWA MFULULIZO

Published By:Mary C. Gwera

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, amewataka Mahakimu kusikiliza kwa mfululizo kesi za jinai ili kupunguza msongamano wa mahabusu, na kuepukana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Jaji Kiongozi alitoa agizo hilo leo alipoanza rasmi ziara ya siku tano ya ukaguzi maalum, Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es salaam.

“Anzeni kusikiliza kesi za jinai mfululizo, itasaidia tusiwe na msongamano wa mahabusu, na wale wanaostahili dhamana wapewe, hatua hii itatuwezesha kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona", alisema Jaji Kiongozi.

Aidha Jaji Kiongozi amewataka watumishi wa Mahakama kuendelea kuepukana na vitendo vya rushwa na kuzingatia maadili ya kazi zao.

Dkt. Feleshi pia amezipongeza Mahakama za Mwanzo kwa kutokuwa na mlundikano wa mashauri.

Katika ziara hiyo Jaji Kiongozi alikagua ujenzi wa jengo la Mahakama ambalo pia litajulikana kama Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki  kilichopo Kinondoni. Jaji Kiongozi pia alikagua Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni, Mahakama ya Wilaya Kinondoni na Mahakama za Mwanzo za Sinza, Kinondoni,Kawe. Kimara, Magomeni na Kariakoo.

Comments (0)

Leave a Comment