Post Details

KAMATI YA BUNGE YAKAGUA MAJENGO YA MAHAKAMA

Published By:LYDIA CHURI

Na Lydia Churi-Mahakama

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imeanza ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa baadhi ya majengo ya Mahakama ya Tanzania ambapo imeridhishwa na miradi ya Kondoa na Manyara iliyokamilika hivi karibuni.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Tabora Mjini Mhe. Emmanuel Mwakasaka ameipongeza Serikali kwa hatua iliyofikiwa ya ukamilishwaji wa ujenzi wa majengo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara pamoja na Mahakama ya Wilaya ya Kondoa.

“Miradi ya ujenzi wa majengo haya imeenda kwa haraka sana, hatukutegemea hili, tumeridhishwa sana na kazi iliyofanyika, pongezi kwa watendaji wote wa Mahakama”, alisema Mhe. Mwakasaka.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara, waaziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa kutekeleza miradi ya ujenzi wa majengo ya Mahakama katika maeneo mbalimbali nchini.

“Kwa hali tuliyoikuta leo inaonesha kuna kazi kubwa imefanyika na muonekano wa jengo sasa ni mzuri, limekamilika,alisema waziri huyo.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imeanza ziara ya kikazi ambapo leo wajumbe wake wamekagua miradi ya ujenzi wa majengo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara na Mahakama ya wilaya ya Kondoa. Kesho wajumbe hao watakagua mradi wa ujenzi wa jengo la Mahakama ya wilaya ya Longido mkoani Ausha.

Comments (0)

Leave a Comment