Post Details

TAARIFA YA MSIBA

Published By:Mary C. Gwera

TANZIA

MAHAKAMA YA TANZANIA INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA, MHE. NATHANIEL MELKIZEDEK MUSHI (pichani) ALIEFARIKI DUNIA MACHI 11, 2020 SAA 7 MCHANA MYUMBANI KWAKE MAILI SITA MOSHI MJINI.

KWA MUJIBU WA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA MSAJILI, MAHAKAMA KUU YA TANZANIA, MHE. SHARMILLAH SARWATT ANASEMA MWILI WA MAREHEMU JAJI MUSHI UNATARAJIWA  KUAGWA NA KUZIKWA  ENEO LA MAILI SITA NYUMBANI KWAKE MJINI MOSHI KILIMANJARO SIKU YA JUMATATU MACHI 16, 2020.

MAREHEMU JAJI MUSHI, ALIZALIWA JULAI 1,1941, ALIAJIRIWA MWAKA 1966 KAMA HAKIMU MKAZI NA KUFANYA KAZI KATIKA MIKOA YA MWANZA NA ARUSHA NA VILEVILE ALIFANYA KAZI ZANZIBAR.

MNAMO JANUARI 01, 1974 ALITEULIWA KUWA HAKIMU MKAZI MKUU NA MWAKA HUOHUO ALITEULIWA KUWA MSAJILI WA MAHAKAMA KUU.

AIDHA; JULAI 27, 1977 MAREHEMU ALITEULIWA KUWA JAJI WA MAHAKAMA KUU NA ALIFANYA KAZI KATIKA VITUO MBALIMBALI KAMA MAHAKAMA KUU, KANDA YA TABORA, MAHAKAMA KUU KANDA YA MOSHI NA BAADAE MAHAKAMA KUU KANDA YA ARUSHA.

MAREHEMU ALISTAAFU RASMI JULAI MOSI, 2001.

MAHAKAMA INATOA POLE KWA FAMILIA NA WOTE WALIOGUSWA NA MSIBA HUU.

MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI, AMINA.

Comments (0)

Leave a Comment