Post Details

MWILI WA JAJI MSTAAFU KAZIMOTO KUZIKWA ALHAMIS DAR ES SALAAM

Published By:LYDIA CHURI

Mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Elias Kazimoto aliyefariki Dunia 

jana mchana unatarajiwa kuzikwa siku ya Alhamis Februari 20, 2020 katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

 

Aidha, mazishi hayo yatatanguliwa na Misa itakayofanyika katika kanisa la Mt. Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es salaam siku hiyo ya Alhamis kuanzia saa 8:00 Mchana.

Msiba wa Marehemu Jaji Kazimoto upo nyumbani kwake Kimara Korogwe jijini Dar es salaam. 

Marehemu Jaji Mstaafu Elias Kazimoto alifariki dunia jana mchana jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Marehemu Jaji Elias Kazimoto alizaliwa Oktoba 9, mwaka 1942 mkoani Morogoro. Aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Januari 6 mwaka 1986.

Alistaafu kazi mwaka 1998 kutokana na ugonjwa.

Comments (0)

Leave a Comment