Post Details

JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA KUU MHE. KAZIMOTO AFARIKI DUNIA

Published By:LYDIA CHURI

Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Elias Kazimoto amefariki Dunia leo mchana jijini Dar es salaam baada ya kuugua muda kwa muda mrefu.

Msiba wa Marehemu Jaji Kazimoto upo nyumbani kwake Kimara Korogwe jijini Dar es salaam na Tarehe ya Mazishi yatafanyika jijini Dar es salaam na tarehe itajulikana hapo baadaye.

Marehemu Jaji Elias Kazimoto alizaliwa Oktoba 9, mwaka 1942.

Aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Januari 6 mwaka 1985

Alistaafu kazi mwaka 1998 baada ya kuugua.

Comments (0)

Leave a Comment