Post Details

SPIKA WA BUNGE AHAIDI KUSHIRIKIANA NA MAHAKAMA

Published By:LYDIA CHURI

Na Lydia Churi- Mahakama Kondoa

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai leo amezindua jengo la Mahakama ya wilaya ya Kondoa na kuahidi kushirikiana na Mahakama ya Tanzania katika kutekeleza Mpango wa miaka mitano wa Maendeleo ya Miundombinu ya Mahakama 2016/17- 2020/21.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo hilo, Spika wa Bunge amesema amefarijika na kuridhishwa na matumizi ya fedha zinazoidhinishwa na Bunge kwa ajili ya Mahakama ambapo ameahidi kushirikiana na Mhimili huo ili kuhakikisha fedha zinazotengwa kwa ajili ya kutekeleza Mpango huo zinapitishwa na Bunge.

Aidha, amewataka watumishi wa Mahakama kulitunza jengo hilo jipya na kutoa huduma bora zinazoendana na jengo hilo zuri na la kisasa kwani wananchi wanaamini watapata haki zao kwa wakati.

Ameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa kujenga jengo bora na la kisasa litakalowezesha matumizi ya Tehama ndani ya Mahakama ambapo alisema hatua hiyo itarahisishsa utendaji kazi na pia kupunguza gharama.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Spika wa Bunge, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahimu Hamis Juma amesema suala la utoaji haki si la Mahakama peke yake bali ni la ushirikiano baina ya Mihimili mingine ambayo huiwezesha Mahakama kutekeleza majukumu yake.

Kuhusu changamoto ya ukosefu na uchakavu wa majengo ya Mahakama, Jaji Mkuu amesema Mahakama imetayarisha Mpango wa miaka mitano wa Mendeleo ya Miundombinu ya Mahakama 2016/17-20202/2021 ili kukabiliana na changoto huiyo. Mpango huo ulioainisha majengo mapya na yatakayojengwa tayari umeshaanza kutekelezwa.

Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, wanananchi wanapojenga hoja za kujengewa jengo la Mahakama wazingatie mazingira tulivu ya uwekezaji na ukuaji wa biashara na hivyo kukuza uchumi wa taifa.

Alitoa wito kwa wananchi kushirikiana Mahakama kwa kujitokeza kutoa ushahidi mahakamani . Jengozuri za Mahalama lililozindiliwa haitakuwa na faida kwama wananchi hawatakubali kutoa ushahidi.

Naye Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Bwn. Mathias Kabunduguru amesema Mahakama ya Tanzania inatarajia kuanza ujenzi wa jengo la Mahakama  Kuu kanda ya Dodoma ambalo litajumuisha ngazi zote za Mahakama  pamoja na ofisi za wadau (Intergrated Justice Centre) hivi karibuni.

Akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa jengo la Mahakama ya wilaya ya Kondoa, Mtendaji Mkuu amebainisha kuwa jengo hilo limejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 679 ambapo kati ya fedha hizo, shilingi milioni 122.25 ni kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

Wakati huo huo, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) Mhe. George Mkuchika amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake waitumie Mahakama kutafuta haki zao.

Comments (1)

  • Photo Loading... Arnold Kirekiano

    THIS IS IT!! HONGERENI SANA WILAYA YA KONDOA NA KANDA YA DODOMA KWA UJUMLA

    31-01-2020

Leave a Comment