Post Details

RAIS MAGUFULI KUZINDUA RASMI MAHAKAMA YA WILAYA- CHATO

Published By:Mary C. Gwera

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAHAKAMA

 

TAARIFA KWA UMMA  

Dar es Salaam: Desemba 17, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli anatarajia kuzindua rasmi jengo la Mahakama ya Wilaya ya Chato.

Uzinduzi huo utafanyika siku ya Jumatano Desemba 18, 2019 kuanzia saa 01:00 asubuhi wilayani humo.

Aidha; Mahakama ya Tanzania inapenda pia kuutaarifu umma kuwa kutakuwa na uzinduzi wa majengo mengine mapya ambayo ni jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi- Mkoa wa Geita pamoja na jengo la Mahakama ya Wilaya ya Bukombe.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma anatarajiwa kufanya uzinduzi wa majengo hayo mawili Desemba 19,  2019 ambapo kuanzia saa 01:00 asubuhi atazindua jengo la  Mahakama ya Wilaya ya Bukombe, na saa 7:00 mchana atazindua jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mkoa wa Geita.

Mahakama ya Tanzania inazindua majengo hayo, lengo likiwa ni kuendelea kusogeza huduma za utoaji haki karibu na wananchi kwa kila ngazi kuanzia ngazi ya Kanda (Mahakama Kuu), Mkoa, Wilaya na Kata (Mahakama za Mwanzo).

Miradi hiyo ya ujenzi inatekelezwa kwa kutumia fedha zinazotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 ‘Mahakama ya Tanzania, pamoja tunaboresha huduma’

Wananchi wote mnakaribishwa,

Imetolewa na:-                       

Mathias B. Kabunduguru

MTENDAJI MKUU

MAHAKAMA YA TANZANIA

Comments (2)

  • Photo Loading... SAFINA M. LUCAS

    NAIPONGEZA MAHAKAMA YA TANZANIA IKIWEMO MIHIMILI PIA KWA KUFANIKISHA HILO HAKI ITAWAFIKIA WANANCHI WA CHATO KWA URAHISI

    18-12-2019
  • Photo Loading... Mgonasipapune

    Hongera kwa Mahakama ya Tanzania kwa jitihada inazochukua katika kuboresha miundombinu yake. Hakika awamu hii ni ya kujivunia kwa kuacha alama kubwa katika maboresho ya miundombinu mbalimbali.

    28-12-2019

Leave a Comment