Post Details

MTENDAJI MKUU-MAHAKAMA AFANYA ZIARA YA KWANZA KIKAZI MANYARA

Published By:Mary C. Gwera

Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru (mwenye shati la bluu bahari) akionyeshwa chumba cha mahabusu ndani ya jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara alipofanya ukaguzi wa jengo hilo mwishoni mwa wiki iliyopita. Hii ni ziara yake ya kwanza kikazi baada ya kuteuliwa na Mhe. Rais hivi karibuni. Aidha, Mtendaji Mkuu huyo amepongeza hatua ambazo jengo hilo limefikiwa na kusisitiza kuwa limalizike haraka kwa ajili ya kuruhusu shughuli za Mahakama ziendelee ipasavyo. 

Hata hivyo, Mtendaji Mkuu amewasisitiza Viongozi wa Mahakama katika mkoa huo kushughulikia upatikanaji wa hati za majengo na viwanja vya Mahakama (kwa maeneo ambayo hayajapata) ili kuweza kuwa na huduma za mahakama katika maeneo ambayo hayana huduma hizo katika Mkoa huo.

Comments (0)

Leave a Comment