Post Details

RAIS SAMIA ATEUA MAJAJI WAPYA 22

Published By:faustine.kapama

  • Wapo watumishi nane wa Mahakama ya Tanzania

Na Faustine Kapama-Mahakama, Morogoro

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameteua maafisa 22 kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi Zuhura Yunus usiku wa kuamkia leo Agosti 6, 2022 imesema uteuzi huo umefanyika Agosti 4, 2022 na wateule hao wataapishwa tarehe itakayotangazwa baadaye.

Walioteuliwa ni Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Kevin Mhina, Wakili Mkuu wa Serikali, Bw. Gabriel Malata, Naibu Msajili wa Mahakama na Katibu wa Jaji Mkuu, Mhe. Adrian Kilimi na Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Happiness Ndesamburo.

Taarifa hiyo imewataja maafisa wengine akiwemo Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Victoria Nongwa, Naibu Msajili na Katibu wa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Obadia Bwegoge na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Mhe. Ruth Massam.

Wengine ni Naibu Msajili na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mhe Godfrey Isaya, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Mhe. Gladys Barthy na Mwendesha Mashitaka Mfawidhi Mahakama Kuu, Zanzibar, Bw. Haji Suleiman Haji.

Uteuzi huo unawajumuisha pia Kamishna Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bi Fatma Khalfan, Wakili wa Serikali, Bw. Abubakar Mrisha na Wakili Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Lusungu Hongoli.

Wengine ni Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bi Monica Otaru, Mkurugenzi Msaidizi (TAMISEMI), Bw. Kamana Kamana, Mkurugenzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Hamidu Mwanga na Mkurugenzi wa Sheria, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marlin Komba.

Uteuzi huo unawajumuisha pia Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Mwajuma Juma, Mhadhiri, Chuo Kikuu Dar es Salaam, Dkt. Cleophas Morris, Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Asina Omari, Wakili wa Kujitegemea, Bi. Aisha Bade na Wakili mwingine wa Kujitegemea, Bw. Mussa Pomo.

Comments (0)

Leave a Comment