Post Details

JAJI MKUU AWAAGIZA VIONGOZI WA MAHAKAMA KUSIMAMIA USAJILI WA KESI MTANDAONI

Published By:LYDIA CHURI

Lydia Churi-Mahakama, Sumbawanga

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Majaji, Naibu Wasajili, Watendaji na Mahakimu wote nchini kutumia mamlaka yao ya usimamizi kuhakikisha wanakagua mfumo wa kusajili na kuratibu mashauri (JSDS II) ili kuona namna mashauri yanavyosajiliwa na kurekebisha endapo kuna makosa.

Jaji Mkuu ametoa agizo hilo kufuatia hatua ya Mahakama ya Tanzania ya kuamua kufanya shughuli zake kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) na kutaka kuacha kupokea takwimu zake kwa njia ya makaratasi na badala yake,  itakuwa ikizisoma takwimu hizo kwa njia ya mtandao.

“Mwaka huu utakuwa ni mwaka wa mwisho kwa Mahakama kupokea takwimu kwenye makaratasi, tutakuwa tukizisoma moja kwa moja kwenye mtandao”, alisema Jaji Mkuu alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akifanya majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu katika mikoa ya Songwe na Rukwa.

“Lengo ni kwenda katika Mahakama ya karne ya 21, Mahakama inayotegemea zaidi mtandao kuliko kutegemea makaratasi”, alisema.

Alisema mfumo wa kusajili na kuratibu mashauri utawawezesha viongozi wa Mahakama kujua ni mashauri mangapi yamesajiliwa nchini, mangapi hayajapangiwa Majaji na Mahakimu, na mangapi yamezidi muda wa kuwepo Mahakamani na hivyo kufuatilia kwa urahisi.

Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, mfumo wa JSDS II utasaidia kuzidisha uwazi katika shughuli za Mahakama na kuongeza imani zaidi ya wananchi kwa Mhimili huo.

Alisema Mahakama imedhamiria kuingia katika Tehama ambapo mwezi Julai mwaka huu iliingia Mkataba wenye thamani ya Sh. bilioni 4.1 na Shirika la Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTCL) utakaowezesha Mahakama kuingizwa kwenye Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano  ambapo majengo 157 ya Mahakama nchini yataunganishwa. 

Mkataba huo utawezesha kuunganishwa kwa majengo ya Mahakama kuanzia Mahakama ya Rufani, Mahakama Kuu,   Mahakama za Hakimu Mkazi, Mahakama za Wilaya na baadhi ya Mahakama za Mwanzo zenye majengo ya kisasa. Mahakama zitakazounganishwa kwenye mtandao huo ni Mahakama ya Rufani 1, Mahakama Kuu  16, Mahakama Kuu Maalumu (Specialized Division 4, Mahakama za Mkoa 29, Mahakama za Wilaya 112 na Mahakama za Mwanzo 10.

Alizitaja faida za Mahakama kusajili mashauri kwa njia ya mtandao kuwa ni pamoja na kuwasaidia mwananchi mwenye shauri Mahakama kufahamu mwenendo mzima wa shauri kwa kujua kila hatua ya shauri lake kwa kufahamu hatua zinazofuata kwenye shauri lake kupitia mtandao.

Jaji Mkuu amehitimisha ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Songwe na Rukwa ambapo alikagua shughuli mbalimbali za Mahakama ikiwemo miradi ya ujenzi wa majengo ya mahakama na hali ya utoaji haki kwa ujumla. Katika ziara hiyo, Jaji Mkuu alikagua ujenzi wa majengo ya Mahakama za Mwanzo za Mlowo mkoani Songwe na Mahakama za Mwanzo za Msanzi na Laela m

Comments (2)

  • Photo Loading... MR.mndeli

    nazani uboreshaji wa huduma ikiwepo kujisajili online ni changamoto, ikiwezekana iwe automatic ili mtu aweze kufanya muda woowote na ata errors iweze ku rectify kwa automatic co adi officer aje kesho kazini bado pia ataa delay ayuko accurate ama active

    15-11-2019
  • Photo Loading... Michael mshani

    Malalamiko ya kesi ya mirathi namba 5/2005

    07-12-2019

Leave a Comment