Post Details

JAJI MKUU MSTAAFU, MHE. JAJI CHANDE AZINDUA MAONESHO YA WIKI YA SHERIA MAHAKAMA KUU KANDA YA DSM

Published By:JoT Admin

Jaji    Mkuu Mstaafu, Mhe.Mohamed Chande Othman amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika Maonesho ya Wiki ya utoaji elimu ya sheria yanayoendelea nchini ili kupata elimu na taratibu mbalimbali za Mahakama.

Kauli hiyo imetolewa leo Februari 02, mwaka huu na  Jaji huyo Mstaafu akiwa mgeni rasmi  wa  siku ya matembezi ya uzinduzi wa Wiki  ya Elimu ya Sheria yanaendelea kufanyika kwenye  Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

“ Natoa wito  kwa wananchi kujitokeza na kushiriki katika maonyesho haya kwani kuna  mambo mengi sana yenye manufaa  katika maisha yetu ya kujifunza na kuyafahamu kwa ustawi  wa shughuli binafsi na taifa kwa ujumla,”alisema   Jaji Mstaafu Othman.

Matembezi hayo yalianzia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kupitia  barabara ya Ocean hadi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “utoaji  haki kwa wakati  wajibu wa Mahakama na wadau”.

Aidha Jaji Mstaafu huyo alisisitiza kwamba   huduma zinazotolewa zielekezwe zaidi maeneo ya vijijini kuliko na wananchi wengi wenye uhitaji   wa msaada wa huduma za kisheria.

Mathalani taratibu ufunguaji mashauri, uendeshaji mashauri rufaa  mamlaka  na taasisi zinazohusika kuwakamata wahalifu, kufanya upelelezi,kuendesha mashauri ya jinai mahakamani, na taratibu za ufunguaji na uendeshaji wa mashauri ya madai mahakamani.

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Beatrice Mutungi alisema elimu ya kisheria itatolewa kwenye vituo  vilivyo mtaani katika Manispaa zote za jiji la Dar es Salaam.

Maonesho haya yanadhimishwa nchini  katika maeneo mbalimbali na kitaifa yanafanyika katika Viwanja vya Nyerere ‘Square’ jijini Dodoma ambapo  Mgeni Rasmi ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.

Kilele cha Maadhimsho kitafanyika  Februari 6,mwaka huu kwenye viwanja vya Chimala na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.John Pombe Magufuli.

Comments (0)

Leave a Comment