Post Details

KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI MAHAKAMA KANDA YA MWANZA CHAFANYIKA MKOANI GEITA.

Published By:Mary C. Gwera

Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi Kanda ya Mwanza ambaye pia ni Jaji Mfawidhi wa Kanda hiyo, Mhe. Jaji Sam Rumanyika amewaasa watumishi wa Mahakama kufanya kazi zinazotoa matokeo chanya kwa wananchi wanaofika Mahakamani kupata Huduma.

 Akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama Kanda ya Mwanza, kilichofanyika Machi 29,2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa- Geita, Mhe. Jaji Rumanyika alisema kuwa kuna baadhi ya Watumishi hawatimizi majukumu yao ipasavyo.

“Nawasihi kuacha tabia ya  kuhudhuria kazini bali mfike kwa ajili ya kutekeleza majukumu yenu” alieleza Mwenyekiti huyo.

Aidha, Mhe. Jaji Rumanyika alisisitiza kuhusu suala la kuondoa mashauri ya mlundikano kuwa  bado ni kipaumbele hivyo lazima jitihada ziendelee kufanyika ili kumaliza mashauri ya aina hiyo yaliopo na kutozalisha upya mashauri yenye umri mrefu.

Pia amewakumbusha menejimenti  kujenga mahusiano mazuri na watumishi waliochini yao ili kuleta ufanisi mahala pa kazi.

Comments (0)

Leave a Comment