Home / Events Photos / Rais Dkt. John Magufuli amuapisha Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania

Rais Dkt. John Magufuli amuapisha Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania

DSC08527

Baadhi ya Viongozi wa Mahakama wa Mahakama ya Tanzania waliohudhuria katika hafla ya uapishwaji wa Mhe. Jaji Mkuu, waliosimama nyuma wa tatu kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga, wa tatu kulia ni Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati, wa kwanza kushoto ni Naibu Msajili Mwandamizi, Mhe. Phocus Bampikya, wa kwanza kushoto ni Msajili-Mahakama Kuu, Mhe. Ilvin Mugeta, katikati ni Mhe. Angelo Mapunda, Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama na wa pili kushoto ni Mhe. Georgina Mulebya, Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.

DSC08516

Baadhi ya Viongozi mbalimbali kutoka Serikalini, Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB).

DSC08511

Baadhi ya Wahe. Majaji wa Mahakama ya Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu wa Tanzania.

DSC08373

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma, akiongea jambo pindi alipopata nafasi ya kutoa neno mara baada ya kuapishwa kwake, Mhe. Prof. Juma amesisitiza juu ya upatikanaji wa haki kwa wakati kwa wananchi wa aina zote.

DSC08449

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe akiongea neno mara baada ya kumuapisha Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Rais amemtaka Mhe. Jaji Mkuu kutetea haki za wanyonge na kupambana na rushwa ili kusukuma gurudumu la maendeleo. aliyeketi wa kwanza kulia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, wa pili kulia ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, wa pili kushoto ni Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Ndugai na wa kwanza kushoto ni Mhe. Katibu Mkuu Kiongozi, Eng. John Kijazi.

DSC08331

Mhe. Rais akimkabidhi hati ya Kiapo huku akimpongeza Mhe Jaji Mkuu wa Tanzania mara baada ya kumuapisha rasmi kushika nafasi hiyo.

DSC08330

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Joseph Magufuli akisaini hati ya kiapo mara baada ya kumwapisha Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania.

2

Baadhi ya Wahe. Majaji wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Wageni wengine waalikwa wakishuhudia kuapishwa kwa Mhe.Jaji Mkuu (hayupo pichani)

1

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mapema Septemba 11, hafla hiyo fupi ya uapishwaji wa Mhe. Jaji Mkuu imefanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam. Mhe. Jaji Mkuu amethibitishwa katika nafasi hiyo ya Ujaji Mkuu baada ya kutumikia nafasi ya Kaimu Jaji Mkuu kuanzia Januari 18, hadi Septemba 10 mwaka huu.

DSC08453