Home / Events Photos / Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania ahitimisha Ziara yake Mkoani Arusha

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania ahitimisha Ziara yake Mkoani Arusha

Jaji-Mkuu1

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akisamiliana na Watumishi wa Mahakama, Kanda ya Arusha alipowasili katika viwanja vya Mahakama Kuu-Arusha kukamilisha ziara yake ya siku mbili mkoani humo.

Jaji-Mkuu2

Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha,Mhe. Kamugisha akimsomea taarifa ya hali ya utendaji kazi wa Mahakama katika mkoa huo. Lengo la ziara ya Mhe. Kaimu Jaji Mkuu katika Kanda hiyo ni kujifunza na kuona hali halisi ya mazingira ya kazi na utekelezaji wa majukumu.

Jaji-Mkuu3

Naibu Msajili, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Mhe. Rumisha (wa kwanza kulia) akimuonesha Mhe. Kaimu Jaji Mkuu, moja ya kumbi za Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha pindi alipokuwa akikagua ofisi mbalimbali za Mahakama ya Mkoa na Mahakama Kuu katika Kanda hiyo.

Mhe. Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Juma akiwa katika Kompyuta Mpakato akikagua Mfumo wa Kuratibu takwimu za Mashauri kwa njia ya Kielektroniki (JSDS) kuhakikisha kama inafanya kazi ipasavyo, pembeni ni Afisa TEHAMA, Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha, Bw. Athuman.

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, akiongea na Mahakimu na Watumishi wengine wa Mahakama (hawapo pichani), katika maongezi yake na Watumishi hao Mhe. Jaji Prof. Juma amewataka na kuwasisitiza Watumishi hao kufanya kazi kwa kuzingatia Maadili ikiwa ni pamoja na kuwa na lugha nzuri kwa Wateja/Wananchi wanaowahudumia. kulia ni Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha na kushoto ni Mhe. Rumisha, Naibu Msajili-Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha.

Mahakimu na Watumishi wengine wa Mahakama wakimsikiliza Mhe. Kaimu Jaji Mkuu alipokuwa akizungumza nao.

Mahakimu na Watumishi wengine wa Mahakama wakimsikiliza Mhe. Kaimu Jaji Mkuu alipokuwa akizungumza nao.

Watumishi wamkimsikiliza kwa makini Mhe. Kaimu Jaji Mkuu (hayupo pichani)

Watumishi wamkimsikiliza kwa makini Mhe. Kaimu Jaji Mkuu (hayupo pichani)

Jaji-Mkuu8

Mtendaji, Mahakama Kuu-Arusha, Bw. Edward Mbara akiwasilisha taarifa ya hali ya utendaji kazi wa Mahakama katika mkoa huo mbele Mhe. Kaimu Jaji Mkuu na Watumishi wa Mahakama, katika taarifa yake Bw. Mbara alikiri kuwa Kanda ya Arusha inakabiliwa na changamoto kubwa ya miundombinu chakavu ya majengo ya Mahakama n.k (picha na Mary Gwera,Arusha)