Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju leo tarehe 27 Oktoba, 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2025 kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Observers for 2025 General Elections). Mazungumzo hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa mikutano-Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.

