MAHAFALI YA CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA LUSHOTO (IJA): Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb), ambaye pia alikuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 18 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto akitoa hotuba Novemba, 23, 2018. Sehemu ya Wahitimu wa Stashahada ya Sheria, katika Mahafali hayo jumla ya Wanafunzi 345 wamehitimu masomo yao katika ngazi ya Stashahada na Astashahada. Sehemu ya Wahitimu wa Astashahada ya Sheria. Meza kuu ikiongozwa na Mhe. Mgeni rasmi (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Wahitimu wa Stashahada ya Sheria. Msajili Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (aliyeketi mbele) akizungumza na Wahe. Majaji kutoka Mahakama Kuu Zhejiang iliyopo nchini China walipotembelea Ofisi ya Mhe. Msajili Mkuu, Novemba 16, ili kujifunza namna mfumo wa utoaji haki wa Mahakama ya Tanzania unavyofanya kazi na pia kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya utoaji haki na sheria, Mhe. Revocati alizungumza na ugeni huo kwa niaba ya Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania. Msajili Mkuu Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (kushoto) akimpatia zawaji mmoja wa Majaji kutoka Mahakama Kuu Zhejiang nchini China, miongoni mwa zawadi walizopatiwa Majaji hao ni pamoja na nakala za vitabu vya Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania wa miaka mitano (5). Msajili Mkuu Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Majaji kutoka Mahakama Kuu Zhejiang nchini China, wa tatu kulia ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Menejimenti ya Mashauri-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Nkya na wa kwanza kulia ni Mtaalamu Mwelekezi wa Mawasiliano-Mahakama ya Tanzania, Dkt. Cosmas Mwaisobwa. Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) yakutana na Mhe. Jaji Mkuu: Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na TPSF imepanga kuwa na Jukwaa la pamoja kujadili masuala ya msingi ya biashara yenye lengo la kukuza uchumi wa Taifa. Pichani ni Mhe. Jaji Mkuu (aliyeketi mbele) akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya TPSF waliomtembelea Mhe. Jaji Mkuu, Novemba 12, 2018. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (pichani) akizungumza na Ujumbe kutoka TPSF na Viongozi wa Mahakama (hawapo pichani) ofisini kwake, Mahakama ya Rufani (T) jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya TPSF, Bw. Salum Shamte (kushoto) akizungumza jambo, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Bw. Godfrey Simbeye. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya (TPSF), wa nne kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Bw. Salum Shamte, wa sita kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Bw. Godfrey Simbeye, wa nne kulia ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga na wa pili kulia ni Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati. MAJAJI WASTAAFU MAHAKAMA KUU-DIVISHENI YA ARDHI WAAGWA KITAALUMA-JAJI KIONGOZI AONGOZA HAFLA HIYO: Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (katikati) akiwa katika hafla ya kuwaaga rasmi Kitaaluma Majaji Wastaafu wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi, kulia ni Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi, Mhe. Gad Mjemmas. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam, Oktoba 19, 2018. Pichani ni sehemu ya Wahe. Majaji wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam waliojumuika pamoja na Mhe. Jaji Kiongozi na Watumishi na Wageni waalikwa kuwaaga rasmi Kitaaluma Majaji Wastaafu wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi. Mhe. Jaji Kiongozi (katikati) akimkabidhi shada la maua, Jaji Mstaafu, Mhe. Jaji Agathon Nchimbi (kushoto) ikiwa ni ishara ya pongezi kwa kumaliza muda wa kazi/kustaafu salama kwa mujibu wa sheria. Kulia  ni Jaji Mstaafu, Mhe. Gad John Mjemmas. Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Tanga, Mhe. Jaji Amir Mruma (aliyesimama) akitoa elimu kwa Wajumbe wa Kamati ya maendeleo ya Kata ya Hale Wilayani Korogwe alipofanya ziara ya ukaguzi wa shughuli za Mahakama Wilayani humo, Oktoba 23, 2018. Pichani ni Wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita wa shule ya Sekondari ya Nyampulukano iliyopo Wilayani Sengerema wakimsikiliza Mhe. Jaji Mkuu (hayupo pichani) alikuwa akizungumza nao, Oktoba 17, 2018 alipokuwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Mwanza kuanzia Oktoba 15-18, 2018. WANAFUNZI WATAKIWA KUWA NA MAADILI MEMA:JAJI MKUU; Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akisalimiana na  Waalimu wa Shule ya Sekondari Nyampulukano iliyopo Wilayani Sengerema alipofika ili kuzungumza na Wanafunzi wa Shule hiyo kuhusu masuala ya maadili alipokuwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Mwanza.

Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (kulia) awasilishiwa Mada kuhusu hali ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitano (2015/2016-2019/2020) wa Mahakama ya Tanzania, anayewasilisha mada hiyo ni Mkuu wa Kitengo hicho, Mhe. Zahra Maruma (kushoto), katikati ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Dkt. Benhajj Masoud.
 

The United Republic of Tanzania (URT) was born on the 26th April, 1964 when the Republic of Tanganyika and the Peoples Republic of Zanzibar united and formed a single country in the name of Tanzania.
The Administration of Justice in Tanzania is an exclusive constitutional mandate of the Judiciary of Tanzania (JOT) vide articles 4, 107A and 107B of the Constitution of the United Republic of Tanzania 1977, Cap. 2 of the Laws. Its history can be traced back to the pre-colonial era, which said history developed gradually depending on the political and economic organization of the society… Read More
 

Event Photos