Home / News / Ziara ya Mhe. Jaji mkuu mikoa ya Tabora na Shinyanga

Ziara ya Mhe. Jaji mkuu mikoa ya Tabora na Shinyanga

st1Ziara ya Mhe. Jaji Mkuu katika mikoa tajwa ililenga katika kujionea hali ya utendaji kazi wa Mahakama katika mikoa hiyo ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha Watumishi wa Mahakama kufanya kazi kwa ufanisi na weledi ili kuboresha
huduma yautoaji haki nchini.Katika ziara yake Mhe. Jaji Mkuu aliambatana na Maafisa na Watendaji kadhaa wa Mahakama kutoka Makao makuu ili kujioneahali ya utendaji kazi ikiwa ni pamoja na kubainisha na kufanyia kazi changamoto ambazo watumishi wanakumbana nazo katika utendaji kazi wa kila siku.Mhe. Jaji Mkuu aliambatana na Naibu Msajili-Mahakama ya Rufani (T), Naibu Msajili-Mahakama Kuu, Mtendaji wa Mahakama Kuu anayeratibu Mahakama Kuu, Mtendaji wa Mahakama za Wilaya na Mikoa na Mtendaji wa Mahakama za Mwanzo nchini.

Bonyeza hapa kupata habari zaidi