Home / News / Waziri Wa Katiba Na Sheria Atembelea Mradi Wa Ujenzi Wa Mahakama Kuu Mkoani Mara

Waziri Wa Katiba Na Sheria Atembelea Mradi Wa Ujenzi Wa Mahakama Kuu Mkoani Mara

Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi ametembelea Mradi wa Ujenzi wa Mahakama Kuu mkoani Mara na kujionea ujenzi huo unavyoendelea .

Akizungumza baada ya kupata taarifa fupi kuhusu ujenzi wa Mahakama hiyo mapema Machi 20, 2018, Prof. Kabudi amewataka Wasimamizi wa Mradi huo kuutangaza kwani uwepo wa  Mahakama Kuu Mkoani Mara utaleta ahueni kubwa kwa wananchi wa mkoa huo ambao walikuwa wanalazimika kwenda Mwanza kutafuta haki zao.

Mhe. Waziri amesema Mahakama hiyo itakapokamilika wananchi wa mkoa wa Mara watapata haki zao kwa wakati ndani ya mkoa wao bila ya kulazimika kwenda umbali mrefu kutafuta haki.

Ujenzi wa Mahakama Kuu mkoani Mara unatekelezwa kupitia Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama wa 2015/2016-2019/2020 ambao unatoa kipaumbele kwa ujenzi wa miuundombinu ya Mahakama nchini ili kusogeza huduma za Mahakama karibu na wananchi.