Home / News / Waheshimiwa majaji wa Mahakam ya Tanzania wafundwa juu ya usikilizaji wa mashauri ya uchaguzi

Waheshimiwa majaji wa Mahakam ya Tanzania wafundwa juu ya usikilizaji wa mashauri ya uchaguzi

Pichani Mhe. Jaji Edward Rutakangwa, Jaji wa Mahakama ya Rufani (T), akifungua warsha ya Wahe. Majaji kwa niaba ya Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania, juu ya ushughulikiaji wa Mashauri ya uchaguzi uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Pichani Mhe. Jaji Edward Rutakangwa, Jaji wa Mahakama ya Rufani (T), akifungua warsha ya Wahe. Majaji kwa niaba ya Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania, juu ya ushughulikiaji wa Mashauri ya uchaguzi uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

JAJI Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman amewataka Majaji nchini kujiandaa na usikilizaji wa mashauri/kesi za uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Hayo yalisemwa katika risala yake iliyosomwa na Mhe. Jaji Edward Rutakangwa, Jaji wa Mahakama ya Rufaa (T) kwa niaba ya Mhe. Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman alipokuwa akifungua rasmi Warsha ya siku mbili (2) ya Uhamasishaji wa Wahe. Majaji juu ya utatuzi wa migogoro ya Uchaguzi “Judges Sensitization Workshop on Electoral Dispute Resolution.” Katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Alisema kuwa warsha hiyo iliyoandaliwa na kudhaminiwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) inalenga katika

kuwajengea uwezo Wahe. Majaji kukabiliana na kesi za uchaguzi na kusaidia Majaji kufanikisha kesi ziende kwa haraka/spidi na kwa haki. “Warsha hii imekuja wakati muafaka ambapo nchi yetu ipo katika mchakato wa kuelekea uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu, hivyo ametoa wito kwa Wahe. Majaji kujiandaa kushughulikia migogoro au mashauri ya uchaguzi,” Alisema Jaji Rutakangwa. Alisema kuwa kwenye uchaguzi hapakosi malalamiko na kusema kuwa Mahakama imejiandaa kushughulikia mashauri yatakayoletwa Mahakamani kwa kasi na kwa haki. “Sisi kama Mahakama tupo tayari kushughulikia mashauri yatakayoletwa Mahakamani kwa kasi na kwa haki, hivyo tunaiomba Serikali kutoa ushirikiano ikiwa ni pamoja na rasilimali fedha zitakazowezesha kumaliza mashauri hayo kwa wakati,” alisisitiza. Kwa upande wake, Bw. Trasias Kagenzi, Mkurugenzi wa Wilaya ya Maswa ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi alisema kuwa Serikali imejiandaa vyema na mchakato mzima wa uchaguzi ambapo kwa sasa zoezi la uandikishaji linaendelea vyema. “Tumejipanga vizuri katika mchakato mzima wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuandaa usafiri, kuwa na wasimamizi wa uchaguzi wa kutosha, hivyo tuna imani kuwa zoezi hili litakwenda vizuri,” Alisema Kagenzi. Warsha hiyo ya siku mbili iliyoanza tarehe. 03.08.2015 na kumalizika tarehe 04.08.2015 imekusanya jumla ya Majaji 46 wa Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu, tayari warsha kama hiyo imeshafanyika kwa kundi lingine la Majaji waliokutana mkoani Arusha lengo likiwa ni kuwajengea uwezo katika usikilizaji wa mashauri ya uchaguzi.

Wahe. Majaji wakiwa katika warsha hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo imedhaminiwa na UNDP.

Wahe. Majaji wakiwa katika warsha hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo imedhaminiwa na UNDP.

 

Washiriki wa warsha Wahe. Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu pamoja na Wadau wa UNDP wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu.

Washiriki wa warsha Wahe. Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu pamoja na Wadau wa UNDP wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu.