Home / Public Notes / TANGAZO LA MPANGO WA KUSIKILIZA MASHAURI YALIYOFUNGULIWA KABLA YA MWAKA 2016

TANGAZO LA MPANGO WA KUSIKILIZA MASHAURI YALIYOFUNGULIWA KABLA YA MWAKA 2016

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAHAKAMA YA RUFANI

 

TANGAZO LA MPANGO WA KUSIKILIZA MASHAURI YALIYOFUNGULIWA KABLA YA MWAKA 2016

Mahakama ya Rufani ya Tanzania inaendelea na mpango wa kusikiliza mashauri yenye muda mrefu. Kwa sasa imepanga kusikiliza mashauri yaliyofunguliwa kabla yam waka 2016. Mpango wa awali wa kusikiliza mashauri yaliyofunguliwa kabla ya mwaka 2015 ulimalizika mafanikio makubwa. Ilifanikiwa kumaliza kesi 435 kati 540 ilizokuwa imepanga kusikiliza zikiwa ni zile zilizofunguliwa kabla ya mwaka 2015.

Ili kufanikisha zoezi la kusikiliza mashauri hayo ni muhimu Wadau wote kushiriki kikamilifu.

Mahakama ya Rufani inawataarifu wadau wote, warufani na warufani ambao majina yao yako kwenye orodha ya mashauri yaliyofunguliwa kabla ya mwaka 2016 na yale ambayo yamepangwa kusikilizwa kwa mwezi Februari, 2018 kujiandaa kwa ajili ya kusikilizwa rufaa hizo. Ndugu wa warufani na warufaniwa waliofariki wanatakiwa kufungua mirathi ili apatikane msimamizi wa mali za marehemu kabla ya tarehe ya kusikilizwa rufaa husika.

Mawakili wenye rufaa zilizotajwa na warufani na warufaniwa wenye tatizo lolote kuhusiana na mashauri hayo wawasiliane na Msajili wa Mahakama ya Rufani au Naibu Msajili kwa njia ya Simu No. 0784-999056 au 0715-444296 au kwa barua pepe rugalemajk@mail.com au mclizy@yahoo.com.

Orodha ya rufaa hizo ni hii hapa. Aidha orodha hii inapatikana katika tovuti ya Mahakama www.judiciary.go.tz na ya chama cha Mawakili (T.L.S) www.tls.or.tz.

Uonapo  tangazo hili mfahamishe yeyote ambaye ametajwa katika orodha hii.

 

Limetolewa na

J. R. Kahyoza

Msajili wa Mahakama ya Rufani

CASES PENDING IN 1ST PHASE

CASES FOR THE SECOND PHASE