Home / News / TANGAZO KWA UMMA-YAH: KANUNI MPYA ZA MADALALI WA MAHAKAMA

TANGAZO KWA UMMA-YAH: KANUNI MPYA ZA MADALALI WA MAHAKAMA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

                                MAHAKAMA                     

TANGAZO KWA UMMA

Mahakama ya Tanzania inapenda kuutaarifu umma kuwa, Kanuni mpya za Madalali wa Mahakama na Wapeleka Nyaraka za Mahakama zilizotolewa kwenye Tangazo la Serikali Na. 363 la mwaka 2017 (The Court Brokers and Process Servers (Appointment Remuneration and Discipline) Rules, GN No. 363 of 2017) zimeanza kutumika rasmi kama zilivyotolewa kwa mujibu wa Sheria. Kanuni hizo zimefuta Kanuni za awali zilizotolewa kwenye Tangazo la Serikali Na. 315 la mwaka 1997 (The Court Brokers and Process Servers (Appointment Remuneration and Discipline) Rules, GN No. 315 of 1997).

Kanuni mpya zimetenganisha Madalali wa Mahakama na Wapeleka Nyaraka za Mahakama na zimetoa vigezo vya waombaji wa Udalali wa Mahakama na Wapeleka Nyaraka za Mahakama ambapo pamoja na vigezo vingine wanapaswa kuwa na kiwango cha chini cha Elimu ya Kidato cha nne na kuendelea au elimu nyingine linganishi na kuhudhuria mafunzo ya cheti cha umahiri (Certificate of competence) katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.

Hivyo ili kuimarisha na kuboresha utendaji kazi wa Mahakama katika utekelezaji wa hukumu tunaomba Madalali wote wa Mahakama na Wananchi wote wenye kukidhi vigezo tajwa hapo juu na wanaokusudia kuomba na kufanya kazi za Udalali wa Mahakama na kusambaza Nyaraka za Mahakama waombe kazi hiyo baada ya kuhudhuria mafunzo stahiki katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA).

 

Imetolewa na

MSAJILI

MAHAKAMA KUU TANZANIA