Home / News / TANGAZO KWA UMMA

TANGAZO KWA UMMA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAHAKAMA YA TANZANIA

TANGAZO KWA UMMA

Mahakama ya Tanzania inapenda kuchukua fursa hii kumpongeza Mhe. Dkt. Gerald Alex Mbonipa Ndika, ambaye kwa sasa ni Jaji wa Mahakama ya Rufani kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (Institute of Judicial Administration-Lushoto), kuanzia tarehe 17 Juni, 2018.

Mhe. Jaji Gerald Ndika anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Jaji (Mstaafu) Mahakama ya Rufani, John A. Mroso, ambaye amemaliza kipindi chake cha uongozi, tunamshukuru kwa mchango wake na kumuombea mapumziko mema na Afya njema.

Jumuiya ya wana Mahakama inamtakia kila la kheri Mhe. Dkt. Ndika kwenye majukumu yake hayo na hasa kipindi hiki cha Programu ya Maboresho ya Mahakama na Chuo cha Uongozi wa Mahakama kama Mhimili muhimu wa mageuzi hayo.

Imetolewa na;

KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO

MAHAKAMA