Home / News / Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awaapisha majaji wateule

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awaapisha majaji wateule

au1Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewaapisha jumla ya Majaji 14 wa Mahakama ya Rufani (T) na Mahakama Kuu, mmoja akiwa ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani na wengine 13 wakiwa Majaji wa Mahakama Kuu.
Hafla hiyo ya uapisho imefanyika mapema leo katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo Mhe. Rais aliwaapisha Majaji walioteuliwa hivi karibuni.
Akiongea na Waandishi wa Habari baada ya hafla ya kuwaapisha, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman alisema kuwa uteuzi wa Majaji hawa utasaidia katika kuharakisha usikilizaji wa mashauri.
“Kuna baadhi ya Kanda za Mahakama kama Mwanza na Bukoba zimeelemewa na mashauri, hivyo idadi ya Majaji hawa wateule utasaidia katika kuharakisha na hatimaye kumaliza mlundikano wa kesi Mahakamani,” Alisema Mhe. Jaji Mkuu.
Aliongeza kuwa Mahakama imejiwekea malengo katika usikilizaji wa Mashauri ambapo hivi sasa Waheshimiwa Majaji wanatakiwa kusikiliza kesi 220 kwa mwaka, na kwa upande wa Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo na Mikoa wanatakiwa kusikiliza kesi 250, hivyo ongezeko la Majaji litasaidia katika kupunguza kazi uliopo.
Alisema kuwa idadi ya Majaji hawa inapelekea ongezeko la jumla ya Majaji 100 wa Mahakama ya Tanzania na kuongeza kuwa Majaji walioteuliwa wana uzoefu mkubwa wa Sheria na ana imani watafanya kazi kwa kuzingatia misingi ya Sheria na taratibu za Mahakama.

Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe. Ignas Paul Kitusi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kabla ya uteuzi Mhe. Kitusi alikuwa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.

Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe. Ignas Paul Kitusi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kabla ya uteuzi Mhe. Kitusi alikuwa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.

Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimuapisha Mhe. Jaji Richard Mziray kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani (T).

Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimuapisha Mhe. Jaji Richard Mziray kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani (T).