Home / News / Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awaapisha Majaji wateule wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu ya Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awaapisha Majaji wateule wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu ya Tanzania

Kuapishwa-Majaji2Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewaapisha jumla ya Majaji 14 wa Mahakama ya Rufani (T) na Mahakama Kuu, mmoja akiwa ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani na wengine 13 wakiwa Majaji wa MahakamaKuu.
Hafla hiyo ya uapisho imefanyika mapema leo katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo Mhe. Rais aliwaapisha Majaji walioteuliwa hivi karibuni.
Akiongea na Waandishi wa Habari baada ya hafla ya kuwaapisha, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman alisema kuwa uteuzi wa Majaji hawa utasaidia katika kuharakisha usikilizaji wa mashauri.
“Kuna baadhi ya Kanda za Mahakama kama Mwanza na Bukoba zimeelemewa na mashauri, hivyo idadi ya Majaji hawa wateule utasaidia katika kuharakisha na hatimaye kumaliza mlundikano wa kesi Mahakamani,” Alisema Mhe. Jaji Mkuu.
Aliongeza kuwa Mahakama imejiwekea malengo katika usikilizaji wa Mashauri ambapo hivi sasa Waheshimiwa Majaji wanatakiwa kusikiliza kesi 220 kwa mwaka, na kwa upande wa Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo na Mikoa wanatakiwa kusikiliza kesi 250, hivyo ongezeko la Majaji litasaidia katika kupunguza kazi ziliopo.
Alisema kuwa idadi ya Majaji hawa inapelekea ongezeko la jumla ya Majaji 100 wa Mahakama ya Tanzania na kuongeza kuwa Majaji walioteuliwa wanauzoefu mkubwa wa Sheria na anaimani watafanyakazi kwakuzingatia misingi ya Sheria na taratibu za Mahakama.

kuapishwakuapishwa2kuapishwa3