Home / Events Photos / MENEJIMENTI YA MAHAKAMA YA TANZANIA YAFANYA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MPANGO MKAKATI WAKE NA MAENDELEO YA MRADI WA MABORESHO WA HUDUMA ZA MAHAKAMA

MENEJIMENTI YA MAHAKAMA YA TANZANIA YAFANYA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MPANGO MKAKATI WAKE NA MAENDELEO YA MRADI WA MABORESHO WA HUDUMA ZA MAHAKAMA

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga (ambaye ni Mwenyekiti) mkutano kuhusu taarifa ya robo ya mwaka kujadili Mpango Mkakati wa mitano na utekelezaji wa mradi wa Maboresho wa Mahakama katika kipindi cha mwaka 2015/2016 hadi 2019/ 2020 akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.

Mkuu wa kitengo cha Usimamzi wa Mradi wa Maboresho ya Mahakama, Mhe. Zahra Maruma akichangia hoja kwenye mkutano huo kuhusu Mpango Mkakati wa Miaka Mitano. 2015/2016 hadi 2019/ 2020).

Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta akichangia jambo kwenye mkutano huo.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu , Edward Nkembo akielezea ripoti hiyo ya robo mwaka ya Mpango Mkakati wa Miaka Mitano katika idara yake.

Msajili wa Makahama ya Rufani Tanzania, Mhe John Kahyoza akielezea jambo kuhusu Mpango Mkakati wa Miaka Mitano (2015/2016 hadi 2019/ 2020).

Msajili Mkuu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati akichangia jambo kwenye mkutano huo.

Wajumbe wakiwa katika Mkutano huo.

Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashauri-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Nkya akitoa taarifa ya Utekelezaji wa majukumu ya Idara yake katika Mkutano huo.

Mkurugenzi wa Mipango na Usimamizi, Mathias Mwang’u akitoa taarifa ya Idara hiyo katika Mkutano wa Tathmini ya Utekelezaji wa Majukumu ya idara hiyo.

Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu kwa Umma na Mawasiliano wa Mahakama , Nurdin Ndimbe a akitoa taarifa ya Idara hiyo katika Mkutano wa Tathmini ya Utekelezaji wa Majukumu.

Mkurugenzi Msaidizi wa Ukaguzi na Maadili-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Warsha Ngh’umbu akitoa taarifa ya Idara hiyo katika Mkutano wa Tathmini ya Utekelezaji wa Majukumu.