Home / News / Makamu wa Rais Afungua Mkutano wa TAWJA

Makamu wa Rais Afungua Mkutano wa TAWJA

IMG_5098 tawja-meeting tawja-mkutano
IMG_5080Makamu  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaagiza  Majaji wanawake  na Mahakimu  wa Wanawake nchini kuendelea kutoa elimu na ujuzi  juu ya haki  za binadamu ili kuwezesha jamii kuepukana na  vitendo rushwa,ikiwemo rushwa ya ngono  na ukatili wa kijinsia.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu huyo wa Rais  aliyasema hayo leo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nane  Mkutano wa Nane wa Mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) uliofanyika jijini Dar es salaam, ambao umehusisha Majaji Wanawake, Mahakimu Wanawake, wakiwemo baadhi Wanaume.

Mkutano huo wenye lengo la kubadilishana uzoefu juu ya masuala ya utoaji haki na hukumu bila ubaguzi. Kauli mbiu ya mkutano huo ni Kuongoza njia kufikia
hitajio la upatikanaji wa haki kwa wote na kwa wakati”

Aliongeza kwamba chama hicho kina wajibu  wa kuhakikisha upatikanaji wa haki  bila ubaguzi , hususan kwa masuala yanayohusu wanawake na watoto ili kuwezesha ustawi wao kwa ujumla na maendeleo ya nchi.

“ Ninakiaagiza Chama  hiki kuendelea kutoa elimu juu ya haki za binadamu katika jamii kwa maafisa wa Mahakama,  watunga sheria na kwa watu  waliathirika na vitendo  vya rushwa  ya ngono na ukatili wa kijinsia kwa kuwa    utoaji wa elimu ndio, utawezesha  upatikanaji wa haki  kwa wakati kwa  jamii inayohitaji ,” alisema Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Aliongeza kwamba chama hicho kina wajibu  wa kuhakikisha upatikanaji wa haki  bila ubaguzi , hususan kwa masuala yanayohusu wanawake na watoto ili kuwezesha ustawi wao kwa ujumla na maendeleo ya nchi.

Aidha Makamu huyo wa Rais amekishukuru Chama cha Majaji Wanawake cha Dunia(IAWJ) kwa michango na msaada wake kwa  TAWJA kwa program ya miaka mitatu ya  ya kupambana na  vitendo vya rushwa ya ngono vinadaiwa kufanywa na baadhi ya watu wenye madaraka.

Alisema   vitendo hivyo vinasababisha baadhi ya wanawake kutopata huduma mbalimbali  zikiwemo za elimu, ajira, haki na huduma nyinginezo.

Makamu wa Rais pia ameipongeza Wizara ya Katiba na Sheria, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia  masuala ya wanawake( na wadau wengine wa TAWJA kwa kuunga mkono mapambano ya aina zote za ubaguzi na ukatili dhidi ya wanawake na watoto nchini.