Home / News / MAHAKIMU WAPYA WAFUNDWA

MAHAKIMU WAPYA WAFUNDWA

Na Magreth Kinabo 

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati amewataka  Mahakimu  walioajiriwa hivi karibuni kujiepusha na vitendo vya rushwa

Kauli hiyo imetolewa leo na Msajili huyo  wakati akifungua  mafunzo  elekezi  kwa Mahakimu hao  yanayofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa  Mahakama  Kuu, jijini Dar es Salaam.

Aidha  Msajili  huyo  aliwataka  Mahakimu hao kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma na kutojihusisha na ulevi, ugomvi na  matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii kwa vitu visivyo kuwa  vya kimaadili.

Kwa  upande  wake Mtendaji  wa Mahakama Kuu  ya Tanzania,Bw. Leonard Magacha aliwataka  mahakimu  hao  kuwa tayari kufanya kazi  katika maeneo waliyopangiwa  hususan vijijini.

“ Nendeni  mkaripoti  maeneo mliyopangiwa, mkafanye   kazi  bila kuchagua maeneo,” alisema Magacha.

Mtendaji huyo   aliwataka Mahakimu hao kujitunza ili waweze kuepukana na maradhi.

Alisema  kwamba  Mahakimu hao wanapaswa kufanya kazi  kwa kujifunza kutoka kwa  watumishi wengine kwenye maeneo waliyopangiwa.

Aliongeza kuwa Mahakimu hao, wanapaswa kujitunza na kuepukana na maradhi.