Home / News / Jaji Mkuu wa Tanzania Amuapisha Rais wa Awamu ya Tano

Jaji Mkuu wa Tanzania Amuapisha Rais wa Awamu ya Tano

jpm3_jpgMhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania amuapisha Mhe. Dr.John Pombe Maghufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar-Es Salaam jana. Sherehe hizo za kumuapisha Rais wa awamu ya Tano zilihudhuriwa na maelfu ya Watanzania na wageni mbalimbali wakiwemo Marais Wanane. Katika hotuba yake fupi Rais wa awamu ya Tano aliwashukuru Watanzania kwa kumchugua, na aliwaomba wote kushirikiana na kuijenga Tanzania mpya bila kujali dini,kabila au vyama.