Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju leo tarehe 17 Oktoba, 2025 amemuapisha Mhe. Hillary Massala Kuzenza kuwa Hakimu Mkazi kwenye ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Mhe. Masaju amemtaka Hakimu huyo kurejea hotuba yake aliyoitoa tarehe 07 Oktoba, 2025 alipowaapisha Mahakimu wenzake wapya.
Uapisho huo umehudhuriwa na Viongozi kadhaa wa Mahakama wakiwemo Kaimu Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Abdi Kagomba, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel, Kaimu Msajili Mkuu ambaye ni Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Herbert George, Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Chiganga Tengwa.
Wengine ni Naibu Msajili Mwandamizi Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Emmanuel Mrangu, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu-Mahakama ya Tanzania, Bi. Beatrice Patrick, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Masjala Kuu, Mhe. Mwajabu Mvungi, Watendaji wa Mahakama Kuu Masjala Kuu, Bw. Humphrey Paya na Bw. Ginaweda Nashon, Mkurugenzi wa Mafunzo ya Kimahakama kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Mhe. Dkt. Patricia Kisinda, Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo Mahakama ya Tanzania, Bi. Patricia Ngungulu na wengine.