Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mapema Septemba 11, 2017, hafla hiyo fupi ya uapishwaji wa Mhe. Jaji Mkuu imefanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam. Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali akitoa neno katika kikao cha Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kikao hicho cha siku mbili kimeanza kufanyika mapema Septemba 15 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (AICC) uliopo jijini Arusha. Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali (katikati) akiendesha kikao cha Majaji Wajaji kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano (AICC) jijini Arusha, wanaoonekana katika picha (wa pili kushoto) ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda Iringa, Mhe. Mary Shangali, wa pili kulia ni Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Mhe. Sekela Moshi, wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein A. Kattanga na wa kwanza kushoto ni Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati. Wahe Majaji Wafawidhi wakiwa katika kikao hicho,wa kwanza kulia ni Mhe. Salvatory Bongole, Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Bukoba, katikati ni Mhe. David Mrango, Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu-Kanda ya Songea, na wa kwanza kushoto, ni Mhe. Firmin Matogolo, Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu-Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.


 Baadhi ya Wahe. Majaji Wafawidhi wakiwa katika kikao hicho.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza, Mhe. Robert Makaramba akichangia katika Mkutano wa Majaji Wafawidhi unaofanyika jijini Arusha, lengo la Mkutano huo ni kujadiliana kwa pamoja juu usikilizaji wa kesi wa haraka na kuondoa mlundikano wa mashauri na hatimaye wananchi waweze kupata haki zao kwa wakati na hatimaye nguzo namba mbili ya  Mpango Mkakati wa Mahakama ya
Upatikanaji na utoaji wa Haki kwa wakati iweze kutekelezeka ipasavyo
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa neno pindi alipokuwa akifunga Mkutano wa Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa-AICC jijini Arusha, Septemba, 15 na 16, 2017. Sehemu ya Wahe. Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu nchini wakimsikiliza kwa makini Mhe. Jaji Mkuu (hayupo pichani) Sehemu ya Wahe. Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu nchini wakimsikiliza kwa makini Mhe. Jaji Mkuu (hayupo pichani) Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania,Mhe. Hussein Kattanga akitoa neno, amesisitiza juu ya ufanyaji kazi kwa malengo. Meza Kuu ikiwa katika picha ya pamoja na Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania mara baada ya kuhitimisha kikao cha siku mbili cha kujadili juu ya mikakati ya kuondosha mashauri ya muda mrefu Mahakamani. aliyeketi katikati ni Jaji Mkuu wa Tanzania,Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, wa pili kushoto ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali, wa kwanza kushotoni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Iringa pia ni Jaji namba moja wa Mahakama Kuu ya Tanzania, wa pili kulia ni Kaimu Jaji Mfawidhi,Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Mhe. Sekela Moshi na wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga. Meza Kuu ikiwa katika picha ya pamoja na Wasajili na Watendaji wa Mahakama. Mkuu wa Kitengo cha Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama,Mhe.Zahra Maruma akitoa mara ya utekelezaji wa kazi mbalimbali za Mradi mbele ya Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Mafundi wakiendelea na kazi ya upakaji rangi katika jengo la Kituo cha Mafunzo linalojengwa Kisutu-Dar es Salaam Baadhi ya Wahe. Majaji wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Wageni wengine waalikwa wakishuhudia kuapishwa kwa Mhe.Jaji Mkuu (hayupo pichani) Mhe. Rais akimkabidhi hati ya Kiapo huku akimpongeza Mhe Jaji Mkuu wa Tanzania mara baada ya kumuapisha rasmi kushika nafasi hiyo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mballimbali wa Serikali, wa tatu kulia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, wa pili kushoto ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, wa tatu kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, wa pili kushoto ni Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Yustino Ndugai, wa kwanza kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi na wa kwanza kulia ni Jaji Mkuu Mstaafu, Mhe. Mohamed Chande Othman. Baadhi  ya Wahe. Majaji wa Mahakama ya Tanzania, wakiwa  katika picha ya pamoja  baada ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu wa Tanzania. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitoa neno mara baada ya kumuapisha rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania, Septemba 11, 2017 Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akitoa neno katika hafla ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Waziri amemuhakikishia Mhe. Rais kuwa Jaji Mkuu Mteule ni Muadilifu na Mchapa kazi hivyo atatekeleza majukumu yake ipasavyo. Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali akitoa neno katika hafla ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Septemba 11, 2017, walioketi katika picha wa kwanza kulia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Samia Suluhu Hassan, wa pili kulia ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, wa pili kulia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai na wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi, Eng. John Kijazi. Jaji Mkuu wa Tanzania akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mhe. Theresia Mahongo wakifunua kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo, Karatu. Uwekaji wa jiwe hilo la msingi ulihudhuriwa na Watumishi wa Mahakama, Wananchi, Viongozi wa dini, Maafisa kutoka serikalini. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli   akisalimiana na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali mara baada ya kuwasili  kwenye viwanja vya Mahakama vya Chimala jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria Maadhimisho  ya siku ya Sheria nchini.
 

The United Republic of Tanzania (URT) was born on the 26th April, 1964 when the Republic of Tanganyika and the Peoples Republic of Zanzibar united and formed a single country in the name of Tanzania.
The Administration of Justice in Tanzania is an exclusive constitutional mandate of the Judiciary of Tanzania (JOT) vide articles 4, 107A and 107B of the Constitution of the United Republic of Tanzania 1977, Cap. 2 of the Laws. Its history can be traced back to the pre-colonial era, which said history developed gradually depending on the political and economic organization of the society… Read More
 

Event Photos