UJENZI WA MAHAKAMA KUU MUSOMA-MARA WAENDELEA VIZURI: Muonekano wa jengo la Mahakama Kuu-Kanda ya Musoma likiendelea kujengwa UJENZI WA MAHAKAMA KUU MUSOMA -MARA, WANANCHI WAFURAHIA MRADI HUO: Muonekano wa upande wa kulia wa jengo hilo Muonekano wa mbele ya jengo hilo UJENZI WA MAHAKAMA KUU MUSOMA-MARA: Mkurugenzi wa Kampuni ya D.F MISTRY& CO (1974) LTD, Eng. Bhavesh akionyesha mchoro wa ramani ya jengo hilo linalojengwa. UJENZI WA MAHAKAMA KUU MUSOMA-MARA: Wahandisi wa Mradi huo wakitoa maelezo ya hatua ya ujenzi waliyofikia kwa katika ujenzi wa jengo hilo, kwa sasa hatua iliyofikiwa ni ujenzi wa ghorofa ya kwanza wa jengo hilo litakalokuwa na ghorofa mbili (2), hatua hii ya ujenzi wa 'floor' ya kwanza itachukua takribani mwezi mmoja hadi kukamilika UJENZI WA MAHAKAMA KUU-MUSOMA WAENDELEA: Mafundi wakiendelea na ujenzi MABORESHO YA MIUNDOMBINU YA MAJENGO YA MAHAKAMA MKOANI MARA- JENGO JIPYA LA MAHAKAMA YA MWANZO-ROBANDA: Pichani ni muonekano wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Robanda lililopo Serengeti wilayani Mugumu, jengo hili lilijengwa kwa nguvu za wananchi na kumaliziwa na Mahakama ya Tanzania lilikabidhiwa rasmi tayari kwa matumizi Januari 26, 2018, uwepo wa jengo hili utasaidia kuwapunguzia wananchi aza ya kusafiri kilomita zipatazo 40 kwenda Mahakama ya Mwanzo Serengeti kutafuta haki zao.
RAIS AWAAPISHA MAJAJI WAWILI WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA ALIOWATEUA FEBRUARI 01, 2018: Jaji Mteule wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. George Mcheche Masaju akizungumza jambo mara baada ya kuapishwa rasmi na Mhe. Rais kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Februari 03, 2018. RAIS AWAAPISHA MAJAJI WATEULE WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Gerson Mdemu kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Hafla ya kuapishwa kwa Majaji Wateule wa Mahakama Kuu ilifanyika Februari 03, 2018 Ikulu jijini Dar es Salaam Jaji Mteule wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Gerson Mdemu akisalimiana na Mhe. Rais mara baada ya kuapishwa, aliyesimama kushoto kwa Mhe. Mdemu ni Jaji Mteule wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. George Mcheche Masaju. Aidha; kwa sasa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mteule ni Mhe. Dkt. Adelardus Kilangi na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni Mhe. Paul Joel Ngwembe.

 UZINDUZI WA MAJENGO MAPYA YA MAHAKAMA YA TANZANIA 'WIKI YA SHERIA NCHINI,2018':Jaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania (pichani) akikata utepe kuzindua rasmi Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo mapema Januari 30, 2018, anayeshuhudia kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Eng. Evarist Ndikilo, jengo hilo la kisasa kabisa lilijengwa kwa kutumia Teknolojia ya Moladi umegharimu jumla ya Tshs.591,837,919, aidha ujenzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya Bagamoyo ulienda sambasamba na ujenzi wa nyumba mbili (2) za Mahakimu zilizogharimu kiasi cha Tshs. 106, 568,514 na kufanya jumla ya kiasi cha 626,406,433 kwa majengo yote ie. Jengo la Mahakama ya Wilaya Bagamoyo pamoja na nyumba mbili. Mhe. Jaji amesema lengo ni kuboresha mazingira bora ya kufanyia kazi ya utoaji haki nchini UZINDUZI WA JENGO JIPYA LA MAHAKAMA YA WILAYA BAGAMOYO, JAN 30,2018: Sehemu ya muonekano wa jengo jipya la Mahakama ya Wilaya Bagamoyo lililozinduliwa mapema Januari 30, 2018 na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma HAFLA YA UZINDUZI WA JENGO JIPYA LA MAHAKAMA YA WILAYA BAGAMOYO:Baadhi ya Watumishi wa Mahakama pamoja na wananchi mbalimbali walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa Mahakama ya Wilaya Bagamoyo: Mahakama hiyo ilizinduliwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma Elimu ya Sheria ikiendelea kutolewa kwa wananchi walipotembelea Viwanjani hapo mapema Januari 27, 2018 siku ambayo Maonyesho yameanza rasmi. Elimu ya Sheria inaendelea nchi nzima, pia kwa upande wa Dar es Salaam, huduma hii inatolewa katika Vituo mbalimbali kama Sinza (Simu 2000-Makmbusho), Magomeni (Manzese-Darajani), Mbezi Mwisho (ndani ya kituo), Kawe Stendi, Tegeta (Stendi Nyuki), Bunju, Mbagala Zakiem, Keko (Keko-Bora), Mjimwema-Kigamboni Stendi, Tandika mbele ya Kituo cha Polisi, Mombasa, Kitunda, Banana, Segerea, Ilala sokoni (Boma), Kariakoo-Msimbazi Polisi, Buguruni Sheli na Gerezani. WIKI YA SHERIA 27-31, JAN, 2018: Muonekano wa Banda la Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa katika Maonyesho ya Wiki ya Sheria nchini, yanayoendelea nchi nzima, Wizara ni Moja ya Taasisi za Sheria zinazoshiriki katika Maonyesho hayo, Taasisi nyingine ni: Tume Ya Utumishi Wa Mahakama, Ofisi Ya Mwanasheria Mkuu Wa Serikali (Agc), Ofisi Ya Mkurugenzi Wa Mashitaka (DPP), Mkemia Mkuu Wa Serikali, TAKUKURU (PCCB), Wakala Wa Usajili, Ufilisi Na Udhamini (Rita) na nyingine nyingi. Maonyesho ya Wiki ya Sheria yaanza rasmi, Kuanzia Januari, 27-Januari 31, 2018: Mkurugenzi wa Malalamiko na Maadili-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Happiness Ndesamburo akisikiliza malalamiko ya mmoja wa wananchi aliyetembelea katika Banda hilo lililopo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma (kushoto) akiwaapisha mawakili wapya, kulia kwake ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali. Baadhi ya Mawakili wakitoa heshima mbele ya Mhe. Jaji Mkuu na Majaji wengine waliopo meza kuu mara baada Mhe. Jaji Mkuu kutamka rasmi kwa mujibu sheria kuwa Mawakili rasmi. Pichani ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akitoa hotuba yake katika Sherehe za Kuwakubali Mawakili Wapya, katika hotuba yake Mhe. Jaji Mkuu amewataka Mawakili hao wapya kutekeleza Majukumu yao kwa mujibu wa sheria na kufuata maadili ya kazi, vilevile amewaasa kutojihusisha na rushwa kwa maana ni adui mkubwa wa haki. Pichani ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju akitoa hotuba yake, katika hotuba yake, Mhe. Masaji amewataka Mawakili hao kufanya kazi mikoani pia ili waweze kuwasaidia kuwawakilisha Wananchi Mahakamani. UJUMBE WA BENKI YA DUNIA WATEMBELEA MAHAKAMA YA TANZANIA: Baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania wakimsikiliza kwa makini, Mkuu wa Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Mradi wa Maboresho ya Mahakama (JDU), Mhe. Zahra Maruma alipokuwa akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania (2015/2016-2019/2020) UJUMBE WA BENKI YA DUNIA UKIPATIWA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MABORESHO YA HUDUMA ZA MAHAKAMA: Mkuu wa Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Mradi wa Maboresho ya Mahakama, Mhe. Zahra Maruma akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama pamoja na Mpango Mkakati wa miaka mitano (2015/16-2019/2010) wa Mahakama ya Tanzania, unaofadhiliwa na Benki ya Dunia Mtaalamu Mwandamizi wa Maboresho ya Utumishi wa Umma kutoka Benki ya Dunia, Bw. Waleed Malik na Mtaalam mwenzake kutoka Benki ya Dunia wakikagua jengo jipya ya Mafunzo la Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto lililojengwa katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jengo hilo limejengwa kwa ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na Ufadhili wa Benki ya Dunia. Muonekano wa jengo la Mafunzo la Chuo cha Uongozi wa Mahakama lililopo Kisutu jijini Dar es Salaam Ukaguzi wa Mradi wa Ujenzi wa jengo la kisasa la Mahakama ya Mwanzo-Kawe UJUMBE WA BENKI YA DUNIA WAISIFU MAHAKAMA KWA KASI NZURI YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MABORESHO:Pichani ni Mtaalamu Mwandamizi wa Maboresho ya Utumishi wa Umma kutoka Benki ya Dunia (WB), Bw. Waleed Malik akizungumza katika kikao cha tathmini na Wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania. Naibu Waziri wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Zhao Dacheng (katikati) akiongea jambo na Mhe. Jaji Mkuu pindi alipomtembelea Desemba 01, 2017. Naibu Waziri wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Zhao Dacheng akipitia nakala ya Kitabu cha Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania (2015/2016-2019/2020) alichozawadiwa na Mhe.Jaji Mkuu wa Tanzania. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akichangia jambo katika majadiliano baina yake na Naibu wa Waziri wa Katiba na Sheria wa China. Baadhi ya Wahitimu wa Astashahada ya Sheria wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania wakati wa mahafali ya 17 ya chuo hicho baada ya kutunukiwa Astashahada zao Mhe. Jaji Mkuu akifurahia zawadi ya picha aliyopatiwa na Mgeni wake.

Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Jaji Dkt. Paul Kihwelo akizungumza kitu wakati wa mahafali ya 17 ya chuo hicho pembeni yake ni a na mgeni rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof Ibrahim Juma UGENI WA NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA WA JAMHURI YA WATU WA CHINA: Picha ya pamoja baada ya Majadiliano: wa nne kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma, katikati ni Naibu Waziri wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Zhao Dacheng, wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga pamoja na Wajumbe waliombatana na Naibu Waziri. Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof Ibrahim Juma akikata utepe kuzindua Jarida la Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto wakati wa mahafali ya 17 ya chuo hicho.

UGENI-NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA WA CHINA: Majadiliano yakiendelea; pichani ni baadhi ya Wajumbe walioambatana na Naibu Waziri huyo, mbali na Wajumbe hao pia kuna Wajumbe kutoka Mahakama ya Tanzania na Wizara ya Katiba na Sheria, wa pili kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga na wa kwanza kushoto ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria-Tanzania. Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Khamis Juma akizungumza na wahatimu na wageni waalikwa katika mahafali ya 17 ya chuo cha uongozi wa Mahakama Lushoto ambapo wahitimu 292 walitunukiwa Stashahada na Astashahada za Sheria Baadhi ya Wahitimu wa Stashahada na Astashahada ya Sheria wakiwa katika Mahafali yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Mhe. Jaji Mkuu amewataka Wahitimu hao kujiendelea kitaaluma ila kuendana na kasi ya utandawazi. Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Mhe.John Mrosso akizngumza wakati wa Mahafali ya 17 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassani akizungumza katika Mkutano wa kumi wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Nchi za Jumuiya ya Madola (CMJA), Makamu wa Rais amewataka Majaji na Mahakimu kutoka katika nchi hizo kupambana na Vitendo vya rushwa. Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa CMJA wakimsikiliza Mgeni rasmi, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (hayupo pichani) Baadhi ya Wahitimu wa Stashahada ya Sheria wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania wakati wa mahafali ya 17 ya chuo hicho baada ya kutunukiwa Stashahada zao Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. David Kenani Maraga, (wa kwanza kushoto) akibadilishana mawazo na Majaji Wakuu wa Tanzania na Zanzibar, katikati ni Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, kulia ni Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Omar Othman Makungu. Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho, kilichofanyika katika Ofisi ya Jaji Mfawishi-Mahakama Kuu –Kanda ya Tabora Wajumbe wakiwa katika kikao cha kusukuma Mashauri kilichofanyika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma, Oktoba 06, 2017 Wakifurahia kwa pamoja mara baada ya kukabidhiwa leseni hiyo. (wa kwanza kulia) ni Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati, katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano-Mahakama ya Tanzania, Bw. Nurdin Ndimbe na wa kwanza kushoto ni Mtendaji-Mahakama ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Uhariri wa Jarida hili, Bw. Samson Mashalla. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahimu Hamis Juma akitoa neno katika ufunguzi wa Mkutano wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Jumuiya ya Nchi za Madola. Katika hotuba yake Mhe. Jaji Mkuu amesisitiza juu ya Maboresho ya huduma za Mahakama nchini na kuahidi kuwa hadi kufikia mwaka 2020 Mahakama ya Tanzania itakuwa imejenga Mahakama za Wilaya 48, Mahakama za Mwanzo 100, Mahakama za Mahakimu Wakazi 14 na Mahakama Kuu 1 na jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania. Washiriki wa Mkutano wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Nchi za Jumuiya ya Madola wakiwa katika Mkutano huo Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga (kushoto) pamoja na Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati wakiwa katika Mkutano huo. Meza Kuu ikiongozwa na Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Nchi za Jumuiya ya Madola. (CMJA) Meza Kuu ikiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Majaji, Mahakimu pamoja na Wasajili Wanawake walioshiriki katika Mkutano huo. Pichani ni Muonekano wa sehemu ya jengo la Mahakama Kuu-Kanda ya Tabora akiongea katika kikao cha Wadau cha kujadili jinsi ya kushirikiana kuondoa mlundikano wa mashauri kufikia Desemba 15, 2017 Pichani ni muonekano wa jengo la Kituo cha Mafunzo cha Mahakama ya Tanzania linalojengwa katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam linalojengwa chini ya Mradi wa Benki ya Dunia (WB), kwa sasa jengo hilo lipo kwa hatua za mwisho za umalizwaji wa wake, ikiwa ni pamoja na uwekaji wa marumaru (tiles), madirisha na milango, pia upakaji wa rangi.
Mhandisi wa Moladi Tanzania, Eng.Steven Hanta amesema kuwa jengo hilo linatarajiwa kukamilika kati ya tarehe 06 mpaka 07, Oktoba, 2017 endapo hakutajitokeza tatizo lolote. Jengo hilo linatarajiwa kufunguliwa rasmi sambasamba na kuanza rasmi kwa mafunzo ya kwanza Oktoba 12, 2017.
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali (katikati) akiendesha kikao cha Majaji Wajaji kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano (AICC) jijini Arusha, wanaoonekana katika picha (wa pili kushoto) ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda Iringa, Mhe. Mary Shangali, wa pili kulia ni Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Mhe. Sekela Moshi, wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein A. Kattanga na wa kwanza kushoto ni Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati. Wahe Majaji Wafawidhi wakiwa katika kikao hicho,wa kwanza kulia ni Mhe. Salvatory Bongole, Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Bukoba, katikati ni Mhe. David Mrango, Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu-Kanda ya Songea, na wa kwanza kushoto, ni Mhe. Firmin Matogolo, Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu-Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mapema Septemba 11, 2017, hafla hiyo fupi ya uapishwaji wa Mhe. Jaji Mkuu imefanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam. Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza, Mhe. Robert Makaramba akichangia katika Mkutano wa Majaji Wafawidhi unaofanyika jijini Arusha, lengo la Mkutano huo ni kujadiliana kwa pamoja juu usikilizaji wa kesi wa haraka na kuondoa mlundikano wa mashauri na hatimaye wananchi waweze kupata haki zao kwa wakati na hatimaye nguzo namba mbili ya Mpango Mkakati wa Mahakama ya
Upatikanaji na utoaji wa Haki kwa wakati iweze kutekelezeka ipasavyo

 Baadhi ya Wahe. Majaji Wafawidhi wakiwa katika kikao hicho.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa neno pindi alipokuwa akifunga Mkutano wa Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa-AICC jijini Arusha, Septemba, 15 na 16, 2017. Sehemu ya Wahe. Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu nchini wakimsikiliza kwa makini Mhe. Jaji Mkuu (hayupo pichani) Sehemu ya Wahe. Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu nchini wakimsikiliza kwa makini Mhe. Jaji Mkuu (hayupo pichani) Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania,Mhe. Hussein Kattanga akitoa neno, amesisitiza juu ya ufanyaji kazi kwa malengo. Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Mkutano wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Jumuiya ya Madola utakaofanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kuanzia Septemba 25-27, 2017. Kushoto ni Jaji Kiongozi waMahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali na kulia ni Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Tanzania Mhe.Jaji Ignas Kitusi.Mhe. Jaji Mkuu ameongelea juu ya Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Jumuiya ya Madola unaotarajiwa kuanza rasmi, Septemba 25, 2017 katika Ukumbi wa Mikutano wa BOT Meza Kuu ikiwa katika picha ya pamoja na Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania mara baada ya kuhitimisha kikao cha siku mbili cha kujadili juu ya mikakati ya kuondosha mashauri ya muda mrefu Mahakamani. aliyeketi katikati ni Jaji Mkuu wa Tanzania,Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, wa pili kushoto ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali, wa kwanza kushotoni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Iringa pia ni Jaji namba moja wa Mahakama Kuu ya Tanzania, wa pili kulia ni Kaimu Jaji Mfawidhi,Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Mhe. Sekela Moshi na wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga. Meza Kuu ikiwa katika picha ya pamoja na Wasajili na Watendaji wa Mahakama. Mkuu wa Kitengo cha Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama,Mhe.Zahra Maruma akitoa mara ya utekelezaji wa kazi mbalimbali za Mradi mbele ya Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Mafundi wakiendelea na kazi ya upakaji rangi katika jengo la Kituo cha Mafunzo linalojengwa Kisutu-Dar es Salaam Sehemu ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mhe. Jaji Mkuu. Baadhi ya Wahe. Majaji wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Wageni wengine waalikwa wakishuhudia kuapishwa kwa Mhe.Jaji Mkuu (hayupo pichani) Mhe. Rais akimkabidhi hati ya Kiapo huku akimpongeza Mhe Jaji Mkuu wa Tanzania mara baada ya kumuapisha rasmi kushika nafasi hiyo. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibarhim Hamis Juma (kulia) akiongea neno na Bw. George Larbi kutoka Benki ya Dunia (katikati) wa kwanza kushoto ni Bw. Denis Biseko 'Co-Team Task Leadear' wa Mradi wa Maboresho ya Huduma za Kimahakama. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mballimbali wa Serikali, wa tatu kulia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, wa pili kushoto ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, wa tatu kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, wa pili kushoto ni Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Yustino Ndugai, wa kwanza kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi na wa kwanza kulia ni Jaji Mkuu Mstaafu, Mhe. Mohamed Chande Othman. Bw. George Larbi, kutoka Benki ya Dunia (WB) (katikati) akiongea na Mhe. Jaji Mkuu (kulia). Baadhi ya Wahe. Majaji wa Mahakama ya Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu wa Tanzania. Mhe. Jaji Mkuu (aliyeketi wa kwanza kulia) akiwa pamoja na Wageni kutoka Benki ya Dunia (wawili walioketi katikati) wa tatu kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga, wa pili kushoto ni Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mradi wa Maboresho wa Huduma za Mahakama, Mhe. Zahra Maruma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitoa neno mara baada ya kumuapisha rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania, Septemba 11, 2017 Ukaguzi: Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Mahakama cha Mahakama-Kisutu unaojengwa kwa fedha za Benki ya Dunia.
Bw. George Larbi kutoka Benki ya Dunia pia alipata fursa ya kutembelea Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Mafunzo cha Mahakama unaofanyika katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa sasa kazi ya upakaji rangi katika jengo hilo inaendelea.

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akitoa neno katika hafla ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Waziri amemuhakikishia Mhe. Rais kuwa Jaji Mkuu Mteule ni Muadilifu na Mchapa kazi hivyo atatekeleza majukumu yake ipasavyo. Jaji Kiongozi-Mahakama Kuu ya Tanzania-Mhe. Ferdinand Wambali akizungumza na Waandishi wa Habari katika Mkutano huo uliofanyika Septemba 21, Katika Ukumbi wa Maktaba-Mahakama ya Rufani (T).

Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali akitoa neno katika hafla ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Septemba 11, 2017, walioketi katika picha wa kwanza kulia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Samia Suluhu Hassan, wa pili kulia ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, wa pili kulia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai na wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi, Eng. John Kijazi. Jaji Mkuu wa Tanzania akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mhe. Theresia Mahongo wakifunua kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo, Karatu. Uwekaji wa jiwe hilo la msingi ulihudhuriwa na Watumishi wa Mahakama, Wananchi, Viongozi wa dini, Maafisa kutoka serikalini.
 

The United Republic of Tanzania (URT) was born on the 26th April, 1964 when the Republic of Tanganyika and the Peoples Republic of Zanzibar united and formed a single country in the name of Tanzania.
The Administration of Justice in Tanzania is an exclusive constitutional mandate of the Judiciary of Tanzania (JOT) vide articles 4, 107A and 107B of the Constitution of the United Republic of Tanzania 1977, Cap. 2 of the Laws. Its history can be traced back to the pre-colonial era, which said history developed gradually depending on the political and economic organization of the society… Read More

News & Events

 

Event Photos

Selected Decisions Relates to Probate & Administration of Estates