JAJI MKUU AWAKUBALI NA KUWAAPISHA MAWAKILI WAPYA 296:Pichani ni sehemu ya baadhi ya Mawakili wapya walioapishwa na Mhe. Jaji Mkuu mapema Desemba 15 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, kufuatia idadi hiyo ya Mawakili wapya inaongeza na kuwa na jumla ya Mawakili 6,536 nchini. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma (kushoto) akiwaapisha mawakili wapya, kulia kwake ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali. Baadhi ya Mawakili wakitoa heshima mbele ya Mhe. Jaji Mkuu na Majaji wengine waliopo meza kuu mara baada Mhe. Jaji Mkuu kutamka rasmi kwa mujibu sheria kuwa Mawakili rasmi. Pichani ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akitoa hotuba yake katika Sherehe za Kuwakubali Mawakili Wapya, katika hotuba yake Mhe. Jaji Mkuu amewataka Mawakili hao wapya kutekeleza Majukumu yao kwa mujibu wa sheria na kufuata maadili ya kazi, vilevile amewaasa kutojihusisha na rushwa kwa maana ni adui mkubwa wa haki. Pichani ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju akitoa hotuba yake, katika hotuba yake, Mhe. Masaji amewataka Mawakili hao kufanya kazi mikoani pia ili waweze kuwasaidia kuwawakilisha Wananchi Mahakamani. UJUMBE WA BENKI YA DUNIA WATEMBELEA MAHAKAMA YA TANZANIA: Baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania wakimsikiliza kwa makini, Mkuu wa Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Mradi wa Maboresho ya Mahakama (JDU), Mhe. Zahra Maruma alipokuwa akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania (2015/2016-2019/2020) UJUMBE WA BENKI YA DUNIA UKIPATIWA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MABORESHO YA HUDUMA ZA MAHAKAMA: Mkuu wa Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Mradi wa Maboresho ya Mahakama, Mhe. Zahra Maruma akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama pamoja na Mpango Mkakati wa miaka mitano (2015/16-2019/2010) wa Mahakama ya Tanzania, unaofadhiliwa na Benki ya Dunia Mtaalamu Mwandamizi wa Maboresho ya Utumishi wa Umma kutoka Benki ya Dunia, Bw. Waleed Malik na Mtaalam mwenzake kutoka Benki ya Dunia wakikagua jengo jipya ya Mafunzo la Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto lililojengwa katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jengo hilo limejengwa kwa ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na Ufadhili wa Benki ya Dunia. Muonekano wa jengo la Mafunzo la Chuo cha Uongozi wa Mahakama lililopo Kisutu jijini Dar es Salaam Ukaguzi wa Mradi wa Ujenzi wa jengo la kisasa la Mahakama ya Mwanzo-Kawe UJUMBE WA BENKI YA DUNIA WAISIFU MAHAKAMA KWA KASI NZURI YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MABORESHO:Pichani ni Mtaalamu Mwandamizi wa Maboresho ya Utumishi wa Umma kutoka Benki ya Dunia (WB), Bw. Waleed Malik akizungumza katika kikao cha tathmini na Wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania. Naibu Waziri wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Zhao Dacheng (katikati) akiongea jambo na Mhe. Jaji Mkuu pindi alipomtembelea Desemba 01, 2017. Naibu Waziri wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Zhao Dacheng akipitia nakala ya Kitabu cha Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania (2015/2016-2019/2020) alichozawadiwa na Mhe.Jaji Mkuu wa Tanzania. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akichangia jambo katika majadiliano baina yake na Naibu wa Waziri wa Katiba na Sheria wa China. Mhe. Jaji Mkuu akifurahia zawadi ya picha aliyopatiwa na Mgeni wake.

UGENI WA NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA WA JAMHURI YA WATU WA CHINA: Picha ya pamoja baada ya Majadiliano: wa nne kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma, katikati ni Naibu Waziri wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Zhao Dacheng, wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga pamoja na Wajumbe waliombatana na Naibu Waziri. UGENI-NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA WA CHINA: Majadiliano yakiendelea; pichani ni baadhi ya Wajumbe walioambatana na Naibu Waziri huyo, mbali na Wajumbe hao pia kuna Wajumbe kutoka Mahakama ya Tanzania na Wizara ya Katiba na Sheria, wa pili kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga na wa kwanza kushoto ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria-Tanzania. Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Khamis Juma akizungumza na wahatimu na wageni waalikwa katika mahafali ya 17 ya chuo cha uongozi wa Mahakama Lushoto ambapo wahitimu 292 walitunukiwa Stashahada na Astashahada za Sheria Baadhi ya Wahitimu wa Astashahada ya Sheria wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania wakati wa mahafali ya 17 ya chuo hicho baada ya kutunukiwa Astashahada zao Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Jaji Dkt. Paul Kihwelo akizungumza kitu wakati wa mahafali ya 17 ya chuo hicho pembeni yake ni a na mgeni rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof Ibrahim Juma Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof Ibrahim Juma akikata utepe kuzindua Jarida la Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto wakati wa mahafali ya 17 ya chuo hicho.

Baadhi ya Wahitimu wa Stashahada na Astashahada ya Sheria wakiwa katika Mahafali yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Mhe. Jaji Mkuu amewataka Wahitimu hao kujiendelea kitaaluma ila kuendana na kasi ya utandawazi. Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Mhe.John Mrosso akizngumza wakati wa Mahafali ya 17 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassani akizungumza katika Mkutano wa kumi wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Nchi za Jumuiya ya Madola (CMJA), Makamu wa Rais amewataka Majaji na Mahakimu kutoka katika nchi hizo kupambana na Vitendo vya rushwa. Baadhi ya Wahitimu wa Stashahada ya Sheria wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania wakati wa mahafali ya 17 ya chuo hicho baada ya kutunukiwa Stashahada zao Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa CMJA wakimsikiliza Mgeni rasmi, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (hayupo pichani) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. David Kenani Maraga, (wa kwanza kushoto) akibadilishana mawazo na Majaji Wakuu wa Tanzania na Zanzibar, katikati ni Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, kulia ni Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Omar Othman Makungu. Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho, kilichofanyika katika Ofisi ya Jaji Mfawishi-Mahakama Kuu –Kanda ya Tabora Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi-Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma, Mhe. Flora Mtarania akiongoza kikao cha Kusukuma Mashauri ‘Case Flow Management Meeting’ kilichofanyika katika Ukumbi wa Mahakama ya Mkoa Kigoma Oktoba 06, 2017 Wajumbe wakiwa katika kikao cha kusukuma Mashauri kilichofanyika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma, Oktoba 06, 2017 Wadau wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kikao cha Kusukuma mashauri ya Mahakama-Mkoani Kigoma Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati (kulia) akikabidhiwa leseni ya uchapishaji wa Jarida la Mahakama kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi-Sehemu ya Usajili wa Magazeti, Idara ya HABARI-MAELEZO, Bw. Patrick Kipangula (wa pili kushoto), wanaoshuhudia zoezi hilo ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano-Mahakama ya Tanzania, Bw. Nurdin Ndimbe (wa pili kulia) na wa kwanza kushoto ni Bw. Samson Mashalla, Mtendaji wa Mahakama, anayeshughulikia Mahakama Kuu ambaye pia ni Mjumbe ya Bodi ya Wahariri (Editorial Board) ya Jarida la Mahakama lijulikanalo kwa jina la ‘HAKI BULLETIN’ linalotarajiwa kuanzishwa hivi karibuni Wakifurahia kwa pamoja mara baada ya kukabidhiwa leseni hiyo. (wa kwanza kulia) ni Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati, katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano-Mahakama ya Tanzania, Bw. Nurdin Ndimbe na wa kwanza kushoto ni Mtendaji-Mahakama ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Uhariri wa Jarida hili, Bw. Samson Mashalla. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahimu Hamis Juma akitoa neno katika ufunguzi wa Mkutano wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Jumuiya ya Nchi za Madola. Katika hotuba yake Mhe. Jaji Mkuu amesisitiza juu ya Maboresho ya huduma za Mahakama nchini na kuahidi kuwa hadi kufikia mwaka 2020 Mahakama ya Tanzania itakuwa imejenga Mahakama za Wilaya 48, Mahakama za Mwanzo 100, Mahakama za Mahakimu Wakazi 14 na Mahakama Kuu 1 na jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania. Washiriki wa Mkutano wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Nchi za Jumuiya ya Madola wakiwa katika Mkutano huo Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga (kushoto) pamoja na Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati wakiwa katika Mkutano huo. Meza Kuu ikiongozwa na Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Nchi za Jumuiya ya Madola. (CMJA) Meza Kuu ikiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Majaji, Mahakimu pamoja na Wasajili Wanawake walioshiriki katika Mkutano huo. Pichani ni Muonekano wa sehemu ya jengo la Mahakama Kuu-Kanda ya Tabora akiongea katika kikao cha Wadau cha kujadili jinsi ya kushirikiana kuondoa mlundikano wa mashauri kufikia Desemba 15, 2017 Pichani ni muonekano wa jengo la Kituo cha Mafunzo cha Mahakama ya Tanzania linalojengwa katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam linalojengwa chini ya Mradi wa Benki ya Dunia (WB), kwa sasa jengo hilo lipo kwa hatua za mwisho za umalizwaji wa wake, ikiwa ni pamoja na uwekaji wa marumaru (tiles), madirisha na milango, pia upakaji wa rangi.
Mhandisi wa Moladi Tanzania, Eng.Steven Hanta amesema kuwa jengo hilo linatarajiwa kukamilika kati ya tarehe 06 mpaka 07, Oktoba, 2017 endapo hakutajitokeza tatizo lolote. Jengo hilo linatarajiwa kufunguliwa rasmi sambasamba na kuanza rasmi kwa mafunzo ya kwanza Oktoba 12, 2017.
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali (katikati) akiendesha kikao cha Majaji Wajaji kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano (AICC) jijini Arusha, wanaoonekana katika picha (wa pili kushoto) ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda Iringa, Mhe. Mary Shangali, wa pili kulia ni Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Mhe. Sekela Moshi, wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein A. Kattanga na wa kwanza kushoto ni Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati. Wahe Majaji Wafawidhi wakiwa katika kikao hicho,wa kwanza kulia ni Mhe. Salvatory Bongole, Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Bukoba, katikati ni Mhe. David Mrango, Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu-Kanda ya Songea, na wa kwanza kushoto, ni Mhe. Firmin Matogolo, Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu-Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mapema Septemba 11, 2017, hafla hiyo fupi ya uapishwaji wa Mhe. Jaji Mkuu imefanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya Wahe. Majaji Wafawidhi wakiwa katika kikao hicho.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza, Mhe. Robert Makaramba akichangia katika Mkutano wa Majaji Wafawidhi unaofanyika jijini Arusha, lengo la Mkutano huo ni kujadiliana kwa pamoja juu usikilizaji wa kesi wa haraka na kuondoa mlundikano wa mashauri na hatimaye wananchi waweze kupata haki zao kwa wakati na hatimaye nguzo namba mbili ya Mpango Mkakati wa Mahakama ya
Upatikanaji na utoaji wa Haki kwa wakati iweze kutekelezeka ipasavyo
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa neno pindi alipokuwa akifunga Mkutano wa Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa-AICC jijini Arusha, Septemba, 15 na 16, 2017. Sehemu ya Wahe. Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu nchini wakimsikiliza kwa makini Mhe. Jaji Mkuu (hayupo pichani) Sehemu ya Wahe. Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu nchini wakimsikiliza kwa makini Mhe. Jaji Mkuu (hayupo pichani) Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania,Mhe. Hussein Kattanga akitoa neno, amesisitiza juu ya ufanyaji kazi kwa malengo. Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Mkutano wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Jumuiya ya Madola utakaofanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kuanzia Septemba 25-27, 2017. Kushoto ni Jaji Kiongozi waMahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali na kulia ni Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Tanzania Mhe.Jaji Ignas Kitusi.Mhe. Jaji Mkuu ameongelea juu ya Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Jumuiya ya Madola unaotarajiwa kuanza rasmi, Septemba 25, 2017 katika Ukumbi wa Mikutano wa BOT Meza Kuu ikiwa katika picha ya pamoja na Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania mara baada ya kuhitimisha kikao cha siku mbili cha kujadili juu ya mikakati ya kuondosha mashauri ya muda mrefu Mahakamani. aliyeketi katikati ni Jaji Mkuu wa Tanzania,Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, wa pili kushoto ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali, wa kwanza kushotoni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Iringa pia ni Jaji namba moja wa Mahakama Kuu ya Tanzania, wa pili kulia ni Kaimu Jaji Mfawidhi,Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Mhe. Sekela Moshi na wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga. Meza Kuu ikiwa katika picha ya pamoja na Wasajili na Watendaji wa Mahakama. Mkuu wa Kitengo cha Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama,Mhe.Zahra Maruma akitoa mara ya utekelezaji wa kazi mbalimbali za Mradi mbele ya Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Mafundi wakiendelea na kazi ya upakaji rangi katika jengo la Kituo cha Mafunzo linalojengwa Kisutu-Dar es Salaam Sehemu ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mhe. Jaji Mkuu. Baadhi ya Wahe. Majaji wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Wageni wengine waalikwa wakishuhudia kuapishwa kwa Mhe.Jaji Mkuu (hayupo pichani) Mhe. Rais akimkabidhi hati ya Kiapo huku akimpongeza Mhe Jaji Mkuu wa Tanzania mara baada ya kumuapisha rasmi kushika nafasi hiyo. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibarhim Hamis Juma (kulia) akiongea neno na Bw. George Larbi kutoka Benki ya Dunia (katikati) wa kwanza kushoto ni Bw. Denis Biseko 'Co-Team Task Leadear' wa Mradi wa Maboresho ya Huduma za Kimahakama. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mballimbali wa Serikali, wa tatu kulia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, wa pili kushoto ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, wa tatu kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, wa pili kushoto ni Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Yustino Ndugai, wa kwanza kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi na wa kwanza kulia ni Jaji Mkuu Mstaafu, Mhe. Mohamed Chande Othman. Bw. George Larbi, kutoka Benki ya Dunia (WB) (katikati) akiongea na Mhe. Jaji Mkuu (kulia). Baadhi ya Wahe. Majaji wa Mahakama ya Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu wa Tanzania. Mhe. Jaji Mkuu (aliyeketi wa kwanza kulia) akiwa pamoja na Wageni kutoka Benki ya Dunia (wawili walioketi katikati) wa tatu kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga, wa pili kushoto ni Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mradi wa Maboresho wa Huduma za Mahakama, Mhe. Zahra Maruma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitoa neno mara baada ya kumuapisha rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania, Septemba 11, 2017 Ukaguzi: Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Mahakama cha Mahakama-Kisutu unaojengwa kwa fedha za Benki ya Dunia.
Bw. George Larbi kutoka Benki ya Dunia pia alipata fursa ya kutembelea Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Mafunzo cha Mahakama unaofanyika katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa sasa kazi ya upakaji rangi katika jengo hilo inaendelea.

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akitoa neno katika hafla ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Waziri amemuhakikishia Mhe. Rais kuwa Jaji Mkuu Mteule ni Muadilifu na Mchapa kazi hivyo atatekeleza majukumu yake ipasavyo. Jaji Kiongozi-Mahakama Kuu ya Tanzania-Mhe. Ferdinand Wambali akizungumza na Waandishi wa Habari katika Mkutano huo uliofanyika Septemba 21, Katika Ukumbi wa Maktaba-Mahakama ya Rufani (T).

Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali akitoa neno katika hafla ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Septemba 11, 2017, walioketi katika picha wa kwanza kulia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Samia Suluhu Hassan, wa pili kulia ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, wa pili kulia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai na wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi, Eng. John Kijazi. Jaji Mkuu wa Tanzania akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mhe. Theresia Mahongo wakifunua kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo, Karatu. Uwekaji wa jiwe hilo la msingi ulihudhuriwa na Watumishi wa Mahakama, Wananchi, Viongozi wa dini, Maafisa kutoka serikalini.
 

The United Republic of Tanzania (URT) was born on the 26th April, 1964 when the Republic of Tanganyika and the Peoples Republic of Zanzibar united and formed a single country in the name of Tanzania.
The Administration of Justice in Tanzania is an exclusive constitutional mandate of the Judiciary of Tanzania (JOT) vide articles 4, 107A and 107B of the Constitution of the United Republic of Tanzania 1977, Cap. 2 of the Laws. Its history can be traced back to the pre-colonial era, which said history developed gradually depending on the political and economic organization of the society… Read More

News & Events

 

Event Photos

Selected Decisions Relates to Probate & Administration of Estates