Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akizungumza na waandishi wa habari alipokutana nao leo. Katika Mkutano huo Mhe. Jaji Mkuu amekitaka Chama cha Mawakili Tanganyika kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria kwani ni Taasisi ya Umma  na si Chama binafsi, kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali, na kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga. Waheshimiwa Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakisubiri kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mapema Aprili 20, 2018 Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Ilvin Mugeta kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Sherehe hizo za kuapishwa jumla ya Majaji 10 wa Mahakama Kuu pamoja na Viongozi wengine wa Sekta ya Sheria zilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Elinaza Luvanda kuwa Jaji wa Mahakama Kuuu ya Tanzania, kabla ya uteuzi huu, Mhe. Luvanda alikuwa Katibu wa  Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Yose Joseph Mlyambina kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Immaculata Kajetan Banzi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Mustapher Siyani kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kabla ya uteuzi Mhe. Siyani alikuwa Naibu Msajili, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Paul Joel Ngwembe kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akifungua Kikao cha Wadau Kujadili kazi ya ulinganisho wa chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA) na Vyuo vingine vya Mafunzo endelevu. Kikao hicho kati ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama na Wadau wa Vyuo vingine vinavyotoa mafunzo endelevu kimelenga katika kujadili uzoefu na nafasi ya ushirikiano wa karibu baina ya Chuo hicho na Vyuo vingine. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Stephen Murimi Magoiga kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.  Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA), Jaji Mstaafu, Mhe. John Mrosso akiongea jambo na Wadau walioshiriki katika kikao hicho, katikati ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma, kushoto ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali. Baadhi ya Wajumbe wa Kikao walioshiriki ni Wawakilishi kutoka Chuo cha Dar es Salaam, Chuo cha Magereza-Kiwira, Chuo Kikuu cha Mzumbe, Ofisi ya Utumishi na Utawala Bora,Chuo cha Kodi n.k, aliyeketi nyuma wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Shaaban Lila. Picha ya pamoja ya ushiriki: aliyeketi katikati ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA), Jaji Mstaafu, Mhe. John Mrosso, wa pili kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Shaaban Lila, wa kwanza kulia ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali na wa kwanza kushoto ni Mhe. Jaji Dkt. Paul Kihwelo, Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA).
 

The United Republic of Tanzania (URT) was born on the 26th April, 1964 when the Republic of Tanganyika and the Peoples Republic of Zanzibar united and formed a single country in the name of Tanzania.
The Administration of Justice in Tanzania is an exclusive constitutional mandate of the Judiciary of Tanzania (JOT) vide articles 4, 107A and 107B of the Constitution of the United Republic of Tanzania 1977, Cap. 2 of the Laws. Its history can be traced back to the pre-colonial era, which said history developed gradually depending on the political and economic organization of the society… Read More