JAJI MFAWIDHI, MAHAKAMA KUU KANDA YA ARUSHA AFANYA ZIARA NGORONGORO, LONGIDO: Pichani Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya wilaya Longido, Mhe. Aziza Temu akimuonesha kitu Mhe. Jaji Mfawidhi wakiwa katika jengo la Mahakama la Wilaya Longido linaloendelea kujengwa. Pichani ni muonekano wa jengo la Mahakama ya Wilaya ya Longido lililopo katika ujenzi. Mhe. Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha alitembelea Mradi huu wa ujenzi kujionea maendeleo yake. MHE. JAJI MKUU AENDELEA NA ZIARA YA UKAGUZI WA MAHAKAMA MKOANI MWANZA:  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Kwimba (hawapo pichani) kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, Mhe. Sam Rumanyika na Kulia ni Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Huduma za kimahakama wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Happiness Ndesamburo. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kwimba baada ya kuzungumza nao Oktoba 17,2018 katika ziara yake ya kukagua shughuli za Mahakama. Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi Ngaga na kulia kwake ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, Mhe. Sam Rumanyika. Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa na viongozi wengine wa Mahakama na Mahakimu wa Mahakama zilizopo wilayani Kwimba mara baada ya kuzungumza nao. WANAFUNZI WATAKIWA KUWA NA MAADILI MEMA:JAJI MKUU; Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akisalimiana na  Waalimu wa Shule ya Sekondari Nyampulukano iliyopo Wilayani Sengerema alipofika ili kuzungumza na Wanafunzi wa Shule hiyo kuhusu masuala ya maadili.

Pichani ni Wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita wa shule ya Sekondari ya Nyampulukano iliyopo Wilayani Sengerema wakimsikiliza Mhe. Jaji Mkuu (hayupo pichani) alikuwa akizungumza nao, Oktoba 17, 2018. JAJI MKUU AANZA ZIARA MKOANI MWANZA KUKAGUA SHUGHULI ZA MAHAKAMA, OKTOBA 15, 2018: Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Nansio-Ukerewe mara baada ya kuzungumza nao. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (aliyesimama mbele) akielezea kuhusu Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama baada ya kumkabidhi kitabu cha Mpango huo Kaimu Mkuu wa wilaya ya Ukerewe ambaye ni Katibu Tawala wa wilaya (DAS) Bwana Focus Majumbi. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika picha ya pamoja na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Pius Msekwa (wa pili kushoto) na Mkewe Mama Anna Abdallah (katikati) alipowatembelea nyumbani kwao Nansio Ukerewe. Wa kwanza kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza Mhe. Sam Rumanyika, wa kwanza kulia ni Msaidizi wa Mhe. Jaji Mkuu ambaye pia Naibu Msajili, Mhe. Adrian Kilimi pamoja na watumishi wengine wa Mahakama ya Tanzania. MAFUNZO KWA MAHAKIMU, WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA YATOLEWA MKOANI TABORA: Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Mhe. Salvatory Bongole (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mahakimu na Wajumbe wa Mabaraza ya Kata wanaoshiriki katika Mafunzo ya siku tatu, Oktoba 08, 2018 hadi Oktoba, 10, 2018. Mhe. Jaji Mfawidhi alifungua rasmi Mafunzo hayo. MAFUNZO KWA MAHAKIMU, WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA YATOLEWA MKOANI TABORA: Sehemu ya Washiriki wakiwa katika Mafunzo hayo, Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mahakama ya Tanzania na kuendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) yameshirikisha Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo wa Mkoani Tabora, Wanasheria wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Mwanasheria Mkuu wa Mkoa pamoja na Wajumbe wa Mabaraza ya Kata. Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (kulia) awasilishiwa Mada kuhusu hali ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitano (2015/2016-2019/2020) wa Mahakama ya Tanzania, anayewasilisha mada hiyo ni Mkuu wa Kitengo hicho, Mhe. Zahra Maruma (kushoto), katikati ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Dkt. Benhajj Masoud.  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho cha Mahakama ya Tanzania Mhe. Zahra Maruma alipokuwa akisisitiza jambo wakati anawasilisha Mada kuhusu Mpango Mkakati wa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama. Mada hiyo iliwasilishwa Septemba 07, 2018. Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Ilvin Mugeta akizungumza na wananchi (hawapo pichani) Agosti 29, wakati wa uzinduzi rasmi wa programu maalum ya Kanda hiyo ya kuzungumza na wateja wake. Wananchi wakimsikiliza kwa makini, Mhe. Jaji Mugeta (hayupo pichani) alipokuwa akizindua rasmi programu ya utoaji elimu kwa wananchi/wateja wa Mahakama Kanda ya Dar es Salaam. Naibu Msajili, Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Joachim Tiganga (kushoto) akizungumza na Wananchi waliokuwepo wakati wa hafla hiyo. MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA SHEREHE YA KUAPISHWA MAJAJI WATATU WATEULE WA MAHAKAMA YA AFRIKA AKIWEMO JAJI ABOUD WA TANZANIA: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika hafla hiyo ya Uapisho ilifanyika Agosti, 27,2018 katika Ofisi za Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu na Watu zilizopo mkoani Arusha. JAJI MKUU WA TANZANIA ATEMBELEWA NA WAKILI MKUU WA SERIKALI AGOSTI, 23, 2018: Pichani ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (kulia) akizungumza jambo na Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Julius Mashamba (katikati), kushoto ni Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi, katika mazungumzo hayo Mhe. Jaji Mkuu ameahidi kuwapa ushirikiano katika utendaji kazi. Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Profesa Ibrahim  Hamis Juma (kulia), akimkabidhi Nakala za Mpango Mkakati wa Mahakama kwa Wakili  Mkuu wa Serikali  Dkt. Julius Mashamba (katikati), kushoto ni  Naibu Wakili Mkuu wa Serikali ,Dkt. Ally Possi.
 

The United Republic of Tanzania (URT) was born on the 26th April, 1964 when the Republic of Tanganyika and the Peoples Republic of Zanzibar united and formed a single country in the name of Tanzania.
The Administration of Justice in Tanzania is an exclusive constitutional mandate of the Judiciary of Tanzania (JOT) vide articles 4, 107A and 107B of the Constitution of the United Republic of Tanzania 1977, Cap. 2 of the Laws. Its history can be traced back to the pre-colonial era, which said history developed gradually depending on the political and economic organization of the society… Read More