UONGOZI MPYA WA BARAZA LA UONGOZI WA TAWLA WAJITAMBULISHA RASMI KWA MHE. JAJI MKUU: Pichani ni Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania, Bi. Tike Mwambipile (kulia) akizungumza jambo na Mhe. Jaji Mkuu wakati Uongozi huo ulipomtembelea Mhe. Jaji Mkuu Ofisini kwake, Mahakama ya Rufani Dar es Salaam. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akiongea jambo na Viongozi wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) hawapo pichani. Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TAWLA), Bi. Athanasia Soka (kushoto) akimueleza jambo Mhe. Jaji Mkuu. Mjumbe wa Baraza la Uongozi wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TAWLA), Bi. Happiness Mchaki (mwenye blauzi wa bluu) akichangia jambo wakati wa mazungumzo kati ya Mhe. Jaji Mkuu na Uongozi wa Chama hicho. Mhe. Jaji Mkuu akikabidhi zawadi mbalimbali kwa Mwenyekiti wa TAWLA, Mhe. Jaji Mkuu pia amewapatia nakala za Mpango Mkakati wa Mahakama. Mhe. Jaji Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa TAWLA, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA, Bi. Tike Mwambipile na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa TAWLA, Bi. Athanasia Soka pamoja na Wajumbe wa Baraza la Uongozi wa Chama hicho waliomtembelea Mhe. Jaji Mkuu. MAHAKAMA YA BIASHARA YAJIPANGA KUTEKELEZA MPANGO MKAKATI KWA VITENDO: Pichani ni Mtendaji, Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara, Bw. Willy Machumu akiongea na Watumishi wa Divisheni hiyo (hawapo pichani) alipokuwa akifungua Mafunzo kuhusu Mahusiano kati ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama na Tathmini ya Utendaji kazi (OPRAS) Watumishi wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Biashara  wamkisikiliza Mtendaji wa Mahakama hiyo kwa makini.

Mchumi Mwandamizi, Mahakama ya Tanzania, Bw. Geofrey Mashafi akitoa Mada kuhusu Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania (2015/2016-2019/2020) kwa Watumishi wa Mahakama ya Biashara. Naibu Msajili, Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara, Mhe. Angelo Rumisha akiongea jambo na Watumishi wa Mahakama hiyo kuhusu Mahusiano kati ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama na Tathmini ya Utendaji kazi (OPRAS) katika Ukumbi wa Mahakama ya Biashara, Agosti 09, 2018 UJENZI WA MAHAKAMA NCHINI WASHIKA KASI: Pichani ni jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma linaoendelea kujengwa, Mtendaji Mkuu pamoja na Maafisa wengine wa Mahakama alioambatana watembelea mradi huu ni mingineyo inayoendelea katika hatua mbalimbali za ujenzi lengo ni kusogeza karibu huduma ya upatikanaji haki kwa Wananchi. Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Bw. Hussein Kattanga (wa nne kulia) katika picha ya pamoja mbele ya jengo la Mahakama Kuu Kigoma linaloendelea kujengwa Pichani ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Kattanga akitoa maelekezo wakati alipotembelea ujenzi wa Mahakama ya Wilaya Kasulu mkoani Kigoma katika ziara yake aliyofanya Wilayani humo Agosti, 08, 2018. Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Bw Hussein Kattanga (wa kwanza kulia) akikagua kiwanja kinachotarajiwa kujengwa Mahakama ya Wilaya Buhigwe ikiwa ni muendelezo wa kusogeza huduma kwa wananchi mkoani Kigoma. MAHAKIMU WAPYA WAAPISHWA: Baadhi ya Mahakimu wapya  wakiapa kiapo cha kutekeleza majukumu yao ya kazi mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania  na  viongozi wengine wa Mahakama (hawapo pichani), jumla ya Mahakimu 51 waliapishwa Julai 28, 2018 katika Ukumbi wa Mahakama Kuu Dar es Salaam. Mahakimu wapya wakiapa mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (hayupo pichani) aliyeongoza kiapo hicho. Jaji Mkuu wa Tanzania,Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma akizungumza na baadhi ya Mahakimu  wapya mara baada ya kuwaapisha.  Kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer  Feleshi na kulia ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati. Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe, Dkt. Eliezer  Feleshi akizungumza jambo na baadhi ya Mahakimu wapya walioapishwa Julai 28, kushoto ni Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha na kulia ni Naibu Msajili Mwandamizi Mahakama Kuu, Masjala Kuu, Mhe Messeka Chaba. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mahakimu wapya aliowaapisha. Viongozi walioketi (wa pili kushoto) ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, (wa pili kulia) ni Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati, (wa kwanza kulia) ni Msajili, Mahakama ya Rufani (T), Mhe. John Kahyoza na (wa kwanza kushoto) ni Mtendaji, Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha. Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (mwenye koti la brown) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Watumishi wa Mahakama walioshiriki kutoa elimu kwa umma katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa, Sabasaba 2018. SHEREHE YA KUWAAGA MAJAJI WAWILI WASTAAFU WA MAHAKAMA YA RUFANI: Jaji Mkuu wa Tanzania aliyeketi upande wa juu kulia akiongoza sherehe ya kuwaaga Majaji wawili Wastaafu wa Mahakama ya Rufani ambao ni Mhe. Jaji Benard Luanda na Mhe. Jaji Sauda Mjasiri, sherehe ya kuwaaga kitaaluma ilifanyika Julai 27, katika Ukumbi namba 1 wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Adelardus Kilangi (kushoto) akiuliza jambo alipokuwa akielezwa na Maafisa wa Mahakama juu ya upatikanaji wa nakala za hukumu kupitia Tovuti ya Mahakama wakati alipotembelea banda la Mahakama ya Tanzania katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa. SHEREHE YA KUAGWA KITAALUMA MAJAJI WAWILI WASTAAFU WA MAHAKAMA YA RUFANI (T)Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (aliyeketi mbele wa kwanza kushoto) pamoja na baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Watendaji na Watumishi wa Mahakama wakiwa katika sherehe hiyo. Mtendaji Mkuu akijadili jambo na Maafisa Habari wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano-Mahakama alipotembelea sehemu hiyo, wakati wa Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa, Sabasaba, 2018.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) na Majaji wastaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Benard Luanda (wa tatu kulia) na Mhe. Sauda Mjasiri wakiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania mara baada ya sherehe ya kuwaaga Mhe. Jaji mstaafu Benard Luanda na Mhe. Jaji mstaafu Sauda Mjasiri. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiteta jambo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, Dkt. Sandie Okoro Majaji Wastaafu wa Mahakama ya Rufani (T) wakiwa katika nyuso za furaha mara baada ya kuagwa rasmi kitaaluma baada ya kustaafu kwa mujibu wa sheria, kushoto ni Mhe. Benard Luanda na kulia ni Mhe. Sauda Mjasiri, na katikati ni mke wa Mhe. Jaji Luanda. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Jaji Ferdinand Wambali kuwa Jaji wa Mahakama yaRufani ya Tanzania, hafla hiyo fupi ya kuapishwa Wahe. Majaji ilifanyika Juni 04, 2018 katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Magufuli (kushoto) akimuapisha, Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan  akifungua Mkutano wa Kimataifa wa Jinsia na Haki uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC jijini Arusha kuanzia Juni 11 hadi Juni 13, 2018. Mkutano wa Kimataifa wa siku tatu wa Jinsia na Haki wafungwa rasmi na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (pichani) Juni 13, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli awaapisha Majaji watatu aliowapandisha vyeo, kushoto ni Mhe. Ferdinand Wambali ambaye ameapishwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, kabla ya uteuzi wake Mhe. Jaji Wambali alikuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, katikati ni Mhe. Jaji Mwanaisha Kwariko ambaye ameapishwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani kabla ya uteuzi wake Jaji Kwariko alikuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, na kulia ni Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi ambaye ameapishwa kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kabla ya uteuzi Jaji Feleshi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa. Mhe. Rais akimuapisha Mhe. Mwanaisha Kwariko kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa maneno ya utangulizi kabla ya kumkaribisha rasmi Mhe. Waziri kufunga rasmi mkutano huo, Mhe. Jaji Mkuu ameishukuru Benki ya Dunia ambayo imeshirikiana kwa karibu na Mahakama kufanikisha Mkutano huo, vilevile amewashukuru Wajumbe wote kwa ujumla wao kushiriki katika Mkutano. Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, Dkt. Sandie Okoro akitoa neno la Shukrani kwa Washiriki wa Mkutano kushiriki katika Mkutano huo na kwa Kamati ya Maandalizi kufanikisha kufanyika kwa Mkutano huo wa Kihistoria
 

The United Republic of Tanzania (URT) was born on the 26th April, 1964 when the Republic of Tanganyika and the Peoples Republic of Zanzibar united and formed a single country in the name of Tanzania.
The Administration of Justice in Tanzania is an exclusive constitutional mandate of the Judiciary of Tanzania (JOT) vide articles 4, 107A and 107B of the Constitution of the United Republic of Tanzania 1977, Cap. 2 of the Laws. Its history can be traced back to the pre-colonial era, which said history developed gradually depending on the political and economic organization of the society… Read More