Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (kushoto) akimkabidhi zawadi maalum kama pongezi aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama ambaye pia ni Jaji Kiongozi Mstaafu, Mhe. Fakih Jundu. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Tume ya Utumishi wa Mahakama, picha hiyo ilipigwa mara baada ya zoezi fupi la kuwapongeza waliokuwa Wajumbe wa Tume hiyo kwa kustaafu na kupandishwa cheo iliyofanyika katika Ofisi ya Mhe. Jaji Mkuu, Mahakama ya Rufani (T), Dar es Salaam. Mhe. Ferdinand Wambali, Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania akisalimiana na baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kuu alipowasili mapema tarehe. 16.08.2016 kujionea hali ya utoaji haki katika Kanda hiyo. Aliyepo nyuma ya Mhe. Jaji Kiongozi ni Mhe. Aishieli Sumari, Jaji Mfawidhi , Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, anayefuata nyuma ya Mhe. Sumari ni Mhe. Mpepo, Naibu Msajili, Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, nyuma yake ni Mhe. Fatuma Massengi, Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha. Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga (kulia) wakiwaonyesha jambo wadau wengine wa Mahakama walipotembelea jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi jijini Dar esa salaam   Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Urambo wakisoma bango lenye ujumbe maalum wa kupambana na rushwa katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya. Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga (kulia) akiwaelezea jambo baadhi ya Makatibu Wakuu na watendaji wakuu wa Wizara na Taasisi za Serikali ambao ni Wadau wa Mahakama ya Tanzania walipotembelea kuona maendeleo ya Maandalizi ya Jengo litakalotumika kuwa Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Sinza jijini Dar es salaam. Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman (katikati) akimuelezea jambo Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga (kulia) alipotembelea jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Sinza jijini Dar es Salaam. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman (katikati) akielezea jambo mbele ya viongozi wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS). Kulia kwa Mhe. Jaji Mkuu ni Mhe. Ferdinand Wambali, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kushoto kwa Mhe. Jaji Mkuu ni Mhe. Jaji Mzuna, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Dodoma Mheshimiwa Mwanaisha Kwariko (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi mbalimbali wa Mahakama ya Tanzania wakati wa Mkutano wa Mahakama ya Tanzania na wadau wake kuhusu Mpango Mkakati mjini Dodoma.
 

The United Republic of Tanzania (URT) was born on the 26th April, 1964 when the Republic of Tanganyika and the Peoples Republic of Zanzibar united and formed a single country in the name of Tanzania.
The Administration of Justice in Tanzania is an exclusive constitutional mandate of the Judiciary of Tanzania (JOT) vide articles 4, 107A and 107B of the Constitution of the United Republic of Tanzania 1977, Cap. 2 of the Laws. Its history can be traced back to the pre-colonial era, which said history developed gradually depending on the political and economic organization of the society… Read More
 

Event Photos